Naibu
waziri wa Kilimo, Omari Mgumba (kushoto) akiongea kwa uchungu kuhusu shamba la miwa la Kigongoni Bagamoyo, ambalo mpaka sasa halijafanyiwa kazi.
...........................................
Naibu
waziri wa Kilimo, Omari Mgumba amekerwa na kitendo cha kuchelewa kuanza
shughuli za upandaji mbegu za miwa
katika kitalu cha Kigongoni ambapo Jeshi la Magereza limeingia mkataba na NSSF.
Akizungumza
na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea vitalu hivyo na kukuta pori
lililotelekezwa, Naibu waziri huyo alisema serikali inatumia muda, na fedha
katika kuanzisha miradi mbalimbali hivyo kila mtu kwenye nafasi yake anapaswa
kutimiza wajibu wake ili kutimiza malengo ya serikali.
Alisema
katika awamu hii ya tano chini ya uongozi wa Rais John Magufuli kila mtu
anapaswa kuwajibika ipasavyo na kuacha ubabaishaji ili dhamira ya Rais ya
kuleta mabadiliko ya kiuchumi iwezi ionekano kwa vitendo.
Aliongeza
kwa kusema kuwa, watendaji wa serikali, na taasisi zake wamekuwa wakifanya kazi
kwa kusua sua ukilinganisha na taasisi binafsi jambo ambalo alisema katika
awamu hii kila atakaejaribu kukwamisha miradi ya serikali hatovumiliwa.
Katika
hatua nyingine Naibu waziri huyo amefurahishwa na shamba la miwa la Bagamoyo
Sugar ambapo miwa yake imestawi vizuri kwaajili ya uzalishaji wa sukari katika
kiwanda cha Bagamoyo sugar kilichopo kata ya Makurunge wilaya ni Bagamoyo.
Alisema
Bagamoyo sugar inastahili pongezi kutokana na uwekezaji wake ambao unaona nia
ya dhati ya uanzishwaji wa kiwanda hicho.
Mratibu wa Kiwanda cha Bagamoyo sugar, Sufiani alisema kiwanda hicho kitakapokamilika kinatarijiwa kuzalisha sukari huku mabaki ya miwa kuzalishia umeme.
Mkuu
wa Gereza la Kigongoni, Mrakibu wa Magereza (SP) Muyengi Bulilo akionyesha
ramani ya shamba la miwa Kigongoni Bagamoyo.
Naibu waziri wa Kilimo, Omari Mgumba (kushoto) akikagua shamba la miwa la Bagamoyo sugar lililopo kata ya Makurunge wilayania Bagamoyo, Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Zainabu Kawawa anaefuata ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Joseph Kakunda.
Mkuu
wa wilaya ya Bagamoyo, Zainabu Kawawa (kulia) akimuonyesha Waziri wa Viwanda,
Biashara na Uwekezaji, Joseph Kakunda shamba la miwa kwaajili ya uzalishaji wa
sukari katika kiwanda cha Bagamoyo sugar.
No comments:
Post a Comment