Mbunge
wa Jimbo la Kibaha vijijini Mkoani Pwani, Hamoud Abuu Juma (kushoto) akikamkabidhi
vifaa tiba Mganga Mkuu wa wilaya ya Kibaha Dkt. Ibrahim Isack.
.......................................
Na Omary
Mngindo, Mlandizi.
MBUNGE wa
Jimbo la Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani Humoud Jumaa, amenunua kontena la fut 40
lenye vifaa vya afya sanjali na vya shule, vyote vikiwa na thamani ya sh. Mil.
400.
Hayo yamebainika
kwenye hafla fupi ya kukabidhi vifaa hivyo kwa Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt.
Ibrahimu Isack, iliyofanyika kwenye Hospitali ya Mlandizi mkoani Pwani,
alivyovinunua kutoka nchini Uingereza.
Akizungumza
baada ya kukabidhi vifaa hivyo, Jumaa alisema kuwa hatua hiyo inalenga
kuboresha upatikanaji wa huduma kwa wananchi, ili kukabiliana na changamoto za
hapa na pale katika sekta hiyo.
Alisema
kwamba katika kontena hiyo mbali ya vifaa tiba, pia kuna vifaa vya shule
ambavyo hivyo vitakabidhiwa kwa wahusika wa shule kwenye Kata mbalimbali
jimboni humo, ambapo vifaa hivyo vitaongeza utendaji kazi kwa walimu na
wanafunzi kupokea masomo.
"Hili
Kontena nimelinunua kutoka nchini Uingereza, kuna vifaa vya Hospitali pamoja na
vya shule, vyote vina thamani ya milioni 400, lengo kuu la vifaa ni kuboresha
sekta ya afya na elimu," alisema Jumaa.
Akizungunzia
changamoto kwenye sekta ya afya, Jumaa alianza kwa kumshukuru Rais Dkt. John
Magufuli kwa dhamira yake njema ya kuhakikisha sekta ya afya inaboreshwa nchi kote,
kwa kutenga fedha na kukabidhi katika Wilaya na mikoa kuboresha Vituo vya afya
pamoja na Hospitali.
Akizungumza
baada ya kupokea vifaa hivyo, Dkt. Isack alianza kwa kumshukuru Mbunge Jumaa
kwa msaada huo uliowafikia kwa wakati mwafaka, huku akisema kwamba vitasaidia
kupunguza kama si kumaliza changamoto kwenye sekta hiyo.
"Hatua
ya Mbunge inaunga mkono juhudi za Rais Dkt. John Magufuli ambaye tangu aingie
madarakani ameonesha dhamira ya kuboreshwa kwa sekta mbalimbali, huku
kipaumbele kikubwa kikiwa kwenye sekta ya afya," alisema Dkt. Isack.
Mbunge
wa Jimbo la Kibaha vijijini Mkoani Pwani, Hamoud Abuu Juma akishusha vifaa tiba kwaajili ya kusambaza kwenye Zahanati na Vituo vya Afya katika jimbo lake.
Sehemu
ya vifaa hivyo vilivyotelwa na Mbunge
wa Jimbo la Kibaha vijijini Mkoani Pwani, Hamoud Abuu Juma kwaajili ya Zahanati na vituo vya Afya katika Jimbo lake.
No comments:
Post a Comment