1.
Ofisi ya Waziri Mkuu
inapenda kuujulisha UMMA wa Watanzania kuwa kumekuwepo na taarifa zilizozua
taharuki baina ya wananchi kupitia mitandao ya kijamii ikiwemo “Whatsapp”
kuhusu Ukaguzi Maalumu utakaohusisha Maafisa kazi kupita nyumba kwa nyumba na
kukagua Mikataba ya Kazi, Mshahara kima cha chini cha Mshahara, Mazingira ya
Kazi, malipo ya Hifadhi ya Jamii na fidia kwa Wafanyakazi wote wakiwemo
wafanyakazi wa majumbani. Aidha, tangazo hilo liliainisha faini ya mil 50 kwa
kutojisajili kwenye mfumo wa fidia kwa wafanyakazi (WCF).
2.
Taarifa
hiyo ilieleza pia kuwa zoezi hilo litaanzia Mkoani Mbeya.
3.
Ofisi
inakanusha taarifa hizo na kuueleza UMMA kuwa wapuuze taarifa hizo kwa kuwa
hazina ukweli wowote na wala hazijatolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi,
Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, ambayo ndio yenye dhamana ya kusimamia Sheria
za Kazi
4.
Ofisi
inawataka watu wanaoeneza taarifa hizo za uongo kuacha upotoshaji huo mara
moja. Aidha, Serikali kupitia vyombo mbalimbali inafuatilia taarifa hizi ili
kubaini chanzo chake na wahusika, ili kuchukua hatua za Kisheria na haki
ionekane inatendeka dhidi yao.
5.
Aidha,
Ofisi inatoa wito kwa Waajiri wote kuendelea kutekeleza Sheria za Kazi kwa
kuwapatia Wafanyakazi wao mikataba na kuwalipa stahiki zao kwa mujibu wa Sheria
ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza katika kaguzi mbalimbali.
No comments:
Post a Comment