Mkurugenzi wa kituo cha Life and Hope ''Sober House
Bagamoyo'' Al-karim Sadrudin Bhanji,(kushoto) akifafanua jambo mara baada ya kuwapokea wageni wake ambao ni kundi la CHRISTAFARI kutoka Mareknai
....................................
Waimbaji
wa nyimbo za injili kundi la CHRISTAFARI kutoka Mareknai wametembelea Kituo cha
Life and Hope ''Sober House Bagamoyo'' kilichopo Bagamoyo Mkoa wa Pwani nchini
Tanzania ili kubadilidhsna mawazo na vijana wanaopata malezi katika kituo
hicho.
Wakiwa
katika kituo hicho wameweza kutuo ushuhuda wao jinsi madawa ya kulevya
yanavyomuathiri mtumiaji kiasi cha kupoteza utu wake, heshima mbele ya jamii,
na wakati mwingine kupoteza maisha.
Wamesema
dawa za kulevya zinastahili kupigwa vita kote duniani ili kunusuru kundi la
kubwa la vijana ambalo limetumbukia kwenye matumizi ya dawa hizo.
Msafara
huo wa vijana kutoka nchi mbalimbali ambao kwa pamoja wanatumia nyimbo
kufikisha ujumbe kwenye jamii wamesema kila binadamu ni mwenye kufanya makosa
lakini ni vizuri unapogundua kuwa umekosea ukajirekebisha na kuacha lile kosa
ambalo umeligundua.
Kijana
Makes kutoka nchini Marekani amesimulia kisa chake cha kutumia dawa za kulevya
na kusema kuwa alianza kidogo kidogo kwa kushawishiwa na rafiki yake mpaka
akazoea.
Alisema
katika matumizi yake ya dawa za kulevya alijikuta amepoteza ubinadamu kiasi cha
kujihisi kama amekaribia kupoteza uhai wake.
Anasimulia
kuwa kuanzia hapo alipata ujasiri wa kuacha matumizi ya dawa za kulevya na
hatimae kujiunga na kundi la CHRISTAFARI ili kufikisha ujumbe wake
Akiendelea
kutoa nasaha kwa vijana wa Kituo cha Life and Hope ''Sober House Bagamoyo'' Makes
alisema njia pekee ambayo vijana kote duniani itawasaidia ni kumrudia Mungu wao
ili waishi katika maadili mema ya kumjua muumba wao sambamba na kusikiliza
ushauri wa wazazi.
Alisema
ukiamua kurudi kwa Mungu wako basi Mungu atakusaidia kufikia lengo kwani
kupoteza nguvu kazi ya vijana ni hasara kwa familia na taifa kwa ujumla.
Kwa
upande wao vijana wanaopata malezi katika kituo cha Life and Hope ''Sober House
Bagamoyo'' wamesema wanaamini nia waliyonayo itapokelewa na Mungu na hatimae
nao watakauwa miongoni mwa watanzania wenye kutoa mchango kwa taifa lao.
Walisema
hakuna aliyetaraji kufika hapo walipofika bali nguvu za shetani zilichukua
nafasi yake kiasi kujiona wao wajanja hali ya kuwa wanapotea.
Wametoa
wito kwa jamii kutumia busara na hekina katika kuwarekebisha vijana
walioathirika na dawa za kulevya huku wakiwataka vijana kujitafakari katika
yale wanayofanya ili wasije kujuta hali yakuwa wamepoteza nguvu na baadhi ya
viungo.
Awali
akiwakaribisha wageni hao Mkurugenzi wa kituo cha Life and Hope ''Sober House
Bagamoyo'' Al-karim Sadrudin Bhanji, alisema kituo hicho kinatoa huduma kwa
vijana walioathirika na aina zote za dawa za kulevya ili kuijenga jamii iwe na
watu wenye nguvu za kufanya kazi.
Alisema
licha ya changamoto wanazokumbana nazo kama kituo wameweza kufanikiwa kutoa
vijana wengi ambao kwa sasa wameungana nafamilia zao wakiwa watu wema wenye
kufanya kazi.
Aliongeza
kwa kuwataka wadau mbalimbali ndani na nje ya nchi kujitokeza kusaidia kituo
hicho ili kiweze kutoa huduma kwa ufanisi zaidi.
Alisema
wapo vijana ambao tayari wametengwa na ndugu zao na wanakimbilia katika kituo
hicho kuomba msaada hali inayowalazimu kuwapokea bila ya kujali gharama za
kuwahudumia.
Makes kutoka nchini Marekani, akielezea madhara ya dawa za kulevya walipotembelea katika cha Life and Hope ''Sober House
Bagamoyo'' hivi karibuni.
Mkurugenzi wa kituo cha Life and Hope ''Sober House Bagamoyo'' Al-karim Sadrudin Bhanji, akiwa katika picha ya pamoja na kundi la CHRISTAFARI kutoka Mareknai
No comments:
Post a Comment