Mkuu wa wilaya ya Muheza
Mhandisi Mwanasha
Tumbo akizungumza wakati akifunga Mashindano ya Kombe la Kabunda Cup
Tumbo akizungumza wakati akifunga Mashindano ya Kombe la Kabunda Cup
........................................
Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga Mwanasha
Tumbo amesema atashirikiana na wanamichezo ili kuhakikisha wanaweza mazingira
mazuri yatakayowezesha kupatikana timu ambayo itaweza kushiriki ligi madaraja ya
juu ikiwemo Ligi kuu.
Mwanasha aliyasema hayo wakati fainali michuano ya
kombe la Kabunda Cup iliyokuwa ikichezwa kwenye viwanja vya Vikonge Mtindiro
wilayani Muheza ambapo alisema ili kuweza kuhakikisha wanafanikisha jambo hilo wataendelea
kuhamasisha vijana kujikita kwenye michezo.
Alisema licha ya kuhamasisha michezo kutokana na
kwamba ni ajira ambayo inaweza kuwainua vijana kuichumi na kupata maendeleo
lakini pia aliwahaidi kuwajengea kiwanja cha mpira chenye matofali ili waweze
kuonyesha umahiri wao na hatimaye wilaya hiyo iweze kupata mafanikio kwenye soka.
“Leo nimekuja hapa kuhimitisha Ligi hii kwanza
nimefurahishwa sana na viwango ambavyo mmekuwa
mkivionyesha kwenye mchezo huu nimeongeza na Diwani wenu hapa na niwahaidi kwamba
nitawajengea kiwanja chenye matofali ili hari ya kushiriki kwenye michezo
muweza kuendelea nayo na tunaamini siku zijazo tutairudisha Muheza kwenye
ramani ya soka “Alisema DC Mwanasha.
Alisema kwamba anafanya hivyo ili kuweza kuchochea
maendeleo ya mchezo huo ambao vijana wakiweka bidii
na nia wanaweza kufika mbali ikiwemo kuitangaza wilaya hiyo lakini pia kupata manufaa kama walivyokuwa Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu ambao wanacheza soka la kulipwa nje ya nchi.
na nia wanaweza kufika mbali ikiwemo kuitangaza wilaya hiyo lakini pia kupata manufaa kama walivyokuwa Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu ambao wanacheza soka la kulipwa nje ya nchi.
Awali akizungumza katika fainali hiyo Katibu
Msaidizi wa Kamati ya Mashindano hayo Salehe Mwinjuma alisema lengo la
mashindano hayo yalikuwa ni kuweza kuinua vipaji vya wachezaji wachanga kwenye
Kata hiyo yaliyoanzishwa na mdau wa michezo Seif Kabunda kwa kushirikisha timu
20 zilizocheza kwa mtindo wa makundi.
Alisema kwamba msimu ujao ligi hiyo itakuwa na
mabadiliko makubwa kutokana na mdhamini wa mashindano hayo kuamua kujipanga
upya na kuja kinyengine lengo kubwa likiwa kuhakikisha michezo inapata
mafanikio.
Katika fainali hiyo timu ya Ushirika FC waliweza
kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 na kutawazwa kuwa mabingwa wapya wa Kombe la
Kabunda Cup baada ya kuibamiza Kwarabuye FC mabao 2-1 katika mchezo wa fainali uliochezwa
kwenye uwanja wa Vikonge Mtindiro na kujiny’akulia kombe na kitita cha
sh.milioni moja .
Katika mchezo huo ambao ulikuwa mkali na wenye
ushindani mkubwa uliohudhuriwa na Mkuu wa wilaya ya Muheza
Mwanasha Tumbo ambaye ndie alikabidhi zawadi kwa washindi kwenye michuano hiyo.
Mwanasha Tumbo ambaye ndie alikabidhi zawadi kwa washindi kwenye michuano hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi
Mwanasha
Tumbo kushoto akimkabidhi Kitita cha Milioni moja Nahodha wa timu ya Ushirika Amiri Nko baada ya timu yao kuibuka na ushindi kwenye michuano ya Kombe la Kabunda Cup kushoto ni Afisa Michezo wa wilaya ya Muheza Anania Sama
Tumbo kushoto akimkabidhi Kitita cha Milioni moja Nahodha wa timu ya Ushirika Amiri Nko baada ya timu yao kuibuka na ushindi kwenye michuano ya Kombe la Kabunda Cup kushoto ni Afisa Michezo wa wilaya ya Muheza Anania Sama
MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi
Mwanasha Tumbo kushoto akimkabidhi Kombe la Ubingwa wa Mashindano ya Kabunda
Cup Nahodha wa timu ya Ushirika Amiri Nko kushoto ni Afisa Michezo wa wilaya ya Muheza Anania Sama.
Katibu Msaidizi wa Kamati
ya Mashindano hayo akisoma risala.
MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi
Mwanasha Tumbo katika akiwa kwenye picha ya pamoja na wachezaji
No comments:
Post a Comment