Na
Hadija Hassan, Lindi
Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rusha (TAKUKURU) Mkoa wa Lindi imesema imekuwa
ikipata wakati mgumu katika kupata ushahidi wa matukio ya Rushwa hali
inayopelekea kushindwa kwenye baadhi ya mashauri ya Rushwa yanayofikishwa
Mahakamani
Hayo
yamesemwa na kaimu kamanda wa Takukuru Mkoa wa Lindi, Naibu Mkuu wa Takukuru
Noel Mseo alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki
iliyopita ofisini kwake kwa lengo la kutoa Taarifa ya utendaji kazi kwa
kipindi cha mwezi Oktoba-Disemba mwaka 2018
Mseo
alisema katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita Taasisi hiyo imeweza kupokea
malalamiko 52 kati ya hayo 27 yalikuwa yanahusu vitendo vya Rushwa huku
taarifa 25 zikihusisha mamlaka zingine
"katika
kipindi hiko pia majarada 3 yalipelekwa makao makuu kwa ajili ya
kuombewa kibali cha Mkurugenzi wa mashitaka(DPP) kuwafikisha watuhumiwa
Mahakamani ambapo mpaka sasa jalada moja limesharudi tayari kwa watuhumiwa hao
kuwafikisha mahakamani" alisema Mseo
Alisema
kwa kipindi cha mwezi oktoba hadi Disemba 2018 Taasisi hiyo
imeshinda kesi tatu(3) na kushindwa kesi (2) na kesi 16zikiwa zinaendelea
katika Mahakama mbalimbali za Mkoa na Wilaya
Hata
hivyo Mseo alieleza sababu zilizochangia kushindwa kwa baadhi ya kesi ni
kutokana na Baadhi ya mashahidi kutokutoa ushahidi madhubuti kwa watu
wanaowafahamu na kuishinao, pamoja na kuwepo na muingiliano wa Kesi za
Rushwa na Kesi zingine kutoka vyombo vingine vya dola, hivyo kufanya kesi
kuchukua muda mrefu na kusababisha gharama za kesi kuwa kubwa.
Pamoja
na mambo mengine Mseo alitumia fulsa hiyo kuwahasa wananchiwa wa Mkoa huo
kuacha maramoja vitendo vinavyojihusisha na Rushwa pamoja na kuwaomba kuendelea
kuwaunga mkono kwa kutoa taarifa za vitendo vya Rushwa kwa kutumia namba113 kwa
kuwa mapambao dhidi ya Rushwa sio ya Takukuru Peke yake bali ni ya jamii mzima.
No comments:
Post a Comment