Tuesday, January 22, 2019

UWT PWANI YALAANI KUKITHIRI MIMBA KWA WANAFUNZI.

 Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Pwani Farida Mgomi akiteta jambo na mmoja wa wajumbe katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya umoja wa wanawake (CCM) mkoa wa Pwani Farida Mgomi akizungumza na baadhi ya wajumbe hawapo pichani.
..............................................................

Na Shushu Joel,Kibaha

JUMUIYA ya umoja wa Wazazi mkoa wa Pwani(UWT) umelaani vitendo vinavyozidi kushamili mkoa humo kwa baadhi ya wanaume kuwapachika mimba wanafunzi wa kike wa  shule za msingi na sekondari na kupelekea kuwakatisha masomo yao.


Vitendo vya Wanaume katika mkoa wa Pwani umeshamili kwa kasi kuwapachika wanafunzi mimba na kuwatelekeza wakiwa na mimba hizo kitu ambacho ni sawa na ukatili kwa watoto hao kutokana na kuwa mara baada ya wanafunzi hao kupatiwa ujauzito utelekezwa bila kupatiwa huduma ya aina yeyote ile.


Akizungumza katika baraza la jumuiya hiyo Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo ya wazazi mkoa wa Pwani Farida Mgomi alisema kuwa mimba za wanafunzi katika mkoa wa Pwani imekuwa ni changamoto kubwa kutokana na kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi hao.


“Mwaka jana jumuiya chini ya mwenyekiti tulifanya ziara katika kila wilaya kwa lengo la kuhamasidsha jumuiya lakini kikubwa kilikuwa ni kuibua mafanikio ya kina mama na mtoto lakini watoto wameonekana kuwa na changamoto nyingi kuliko kinamam kutokana na hali wanazokumbana nazo shuleni na mitaani na hali hii imepelekea kuongezeka kwa dimbwi la mimba za wanafunzi hao”Alisema Mgomi.


Aliongeza kuwa takwimu zinaonyesha kuwa mkoa mzima wanafunzi waliokatishwa masomo kwa kupachikwa mimba ni 235 huku wilaya ya mkuranga ikiwa kinara kwa wanafunzi 48,chalinze 46,kisarawe 36,Kibiti 33,Rufiji 21,Kibaha17,Bbagamoyo 10-,Mafia 8 na Kibaha vijijini7.


Aidha Mgomi aliongeza kuwa wingi wa wanafunzi hao kupatiwa mimba ni changamoto kubwa inayowahusu wanawake kutokana na kuwa mzazi wa kike ndiye yuko karibu zaidi na mtoto wa kike pindi anapofikia umri fulani.


“Wazazi wetu walitupatia elimu ya kutosha tangu tukiwa wadogo kwa kusema kuwa tujitahidi katika masomo ili tuje tuisaidie nchi yetu hivyo walitutaka kuepukana na vishawishi kutoka kwa wanaume ili tusome,lakini watoto cha ajabu wazazi wa leo wanashindwa kutoa elimu majumbani kwa watoto wa kike na kuwaachia walimu peke yao”Alisema.


Aliongeza kuwa wameiomba serikali ya mkoa kuhakikisha wanapambana na jambo hili ili kuhakikisha wanatokomeza jangahili katika mkoa ili wanafunzi wa kike waweze kuitimu masomo yao na kulisaidia taifa hili kwa miaka ya mbele.


Naye Fatma Mkoga alipopewa nafasi ya kuzungumza alisema kuwa jumuiya inapambana sana na wale wanaokatisha wanafunzi masomo ili kuhakikisha inawachukulia hatua kali za kisheri akwani inasababisha taifa kukosa wasomi wa baadae kwa kuwadanganyia chipsi tu.


Aidha amempongeza mwenyekiti wa UWT kwa kuonyesha hisia zake katika kuhakikisha jambo hili linakuwa ni kikomo kutokea katika mkoa wa Pwani.


Kwa upande wake Naibu Waziri wa Nishati Subra Mgalu amemuhakikishia mwenyekiti wa jumuiya hiyo kuwa suala hilo sasa liko mahali pake cha msingi ni ushirikiano tu baina ya wazazi na watoto ambao ndio wamekuwa wakipewa ujauzito na wanaume.


Aliongeza kuwa kutokana na uwingi wa idadi ilitajwa na mwenyekiti kwa watoto wetu kuachishwa masomo sasa serikali ya mkoa imelivalia njuga jambo hilo kwa kusema kuwa kila atakayebainika kumpatia mwanafunzi mumba cha moto atakiona.


No comments:

Post a Comment