NA
MWAMVUA MWINYI, PWANI
WAKALA
wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoani Pwani ,unatarajia kutumia kiasi cha
sh.bilioni 25.4 kwa ajili ya kufanya matengenezo mbalimbali ya barabara kwa
bajeti ya mwaka 2018-2019.
Hayo
yalisemwa mjini Kibaha na meneja wa TANROADS mkoani hapo, mhandisi Yudas
Msangi, wakati wa kikao cha bodi ya barabara cha mkoa huo .
Alieleza,
hadi kufikia septemba 2018 zimepokelewa kiasi cha sh. milioni 958.7 kwa
ajili ya matengenezo mbalimbali.
“Katika
kipindi hicho kiasi cha shilingi bilioni 2 zimetumika kufanya matengenezo
mbalimbali kwenye barabara kuu”,
“Kazi
za matengenezo zilichelewa kuanza kutokana na taratibu za manunuzi na uhakiki
wa mikataba ambavyo huchukua muda mrefu kukamilika hasa mikataba inayohakikiwa
kwa mwanasheria mkuu wa serikali”alisema Msangi.
Aidha
Msangi alibainisha, mkoa umepanga kufanya miradi ya maendeleo ya barabara zenye
urefu wa kilometa 32.5 zenye thamani ya sh.bilioni 2.3.
Alisema,meneja
huyo alisema kwenye miradi hiyo ya maendeleo sh. bilioni 1.3 ni bajeti ambapo
sh.milioni 969 ni kutoka mfuko wa barabara vilevile bilioni 7.5 ni kutoka
serikali zitafanya ukarabati kwa kiwango cha changarawe/udongo.
Nae
mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo alieleza, ili kuboresha
barabara za mkoa huo watendaji wanapaswa kuwa waadilifu.
“Kutokana
na mkoa kuwa na viwanda vingi uboreshaji wa miundombinu ya barabara utasaidia
kuinua uchumi wa wananchi na Taifa”:” Pia Muwe makini na baadhi ya watu
wanaoharibu miundombinu ya barabara ,” alisema Ndikilo.
No comments:
Post a Comment