Mkuu
wa Wilaya ya Lindi Shahibu Ndemanga akizungumza na wajasiliamali.
................................................
Na
Hadija Hassan, Lindi
Mkuu
wa Wilaya ya Lindi Shahibu Ndemanga amewataka wajasiliamali wa Wilaya hiyo
kuchangamkia fulsa ya ubanguaji wa korosho iliyotolewa na Serikali
ili waweze kujikwamua kiuchumi
Ndemanga
ameyasema hayo Leo alipokuwa anafunga mafunzo ya ubanguaji bora wa korosho
yaliyotolewa na shirika la kuhudumia viwanda vidogo vidogo Sido mkoa wa Lindi
yaliyofanyika Mjini hapo
Ndemanga
alisema Serikali ilipoamua korosho zote zibanguliwe ndani ya Nchi ilikuwa na
lengo la kuinua uchumi wa Wananchi wake
Alisema
uamuzi wa Sido wa kuwakusanya Wajasiliamali na kuwapa mafunzo ya ubanguaji bora
wa korosho ni kitendo cha kizalendo kwani kutawafanya wajasiliamali hao
kuanzisha viwanda vidogo vidogo vya ubanguaji vitakavyoweza kuwaongezea
vipato vyao
Kwa
upande wake Afisa uendelezaji mafunzo kutoka katika shirika hilo la Sido
Aizack Daniely alisema kuwa katika mafunzo hayo ya siku tano yenye
Lengo la kuongeza kasi ya uongezaji wa thamani katika zao la korosho
ili wananchi waweze kupata kipato kupitia ubanguaji na kutoa ajira kwa jamii,
jumla ya wajasiliamali 48 wameshiriki kutoka wilaya za Lindi na
Nachingwea wakiwemo wanawake 15na wanaume 33
Danieli
alisema katika mafuzo hayo washiriki walipata fulsa ya kujifunza hatua za
ubanguaji bora wa korosho , Teknolojia na ubanguaji bora na usalama na Afya
kiwandani
Aliyataja
mambo mengine kuwa ni ubora , usalama na usafi wa chakula (korosho)
katika uzalishaji, utumiaji na matengenezo madogo
madogo katika mashine za ubanguaji ,upangaji wa madaraja
pamoja na ufungashaji na utunzaji wa madaraja kwa korosho
zilizobanguliwa
Nae
Meneja wa Sido mkoani hapo Mwita Kasisi alisema kuwa Mafunzo hayo yataendelea
kufanyika katika wilaya zingine kulingana na mahitaji ya wilaya husika
Kasisi
aliongeza kuwa baada ya mafunzo hayo washiriki wataweza kupata ajira kutokana
na viwanda vya ubanguaji wa korosho vitakavyofunguliwa na wengine
watakwenda kuanzisha viwanda vyao ambavyo vitatengeneza ajira kwa wananchi wengine
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Wabanguaji Wadogo wadogo Mkoa wa
Lindi, mwalimu mstaafu Mariamu Kaisi alisema kuwa mafunzo hayo
yatawasaidia kuongeza kasi ya utendaji kazi tofauti na awali walipokuwa
wanabangua korosho hizo kwa mazoea
Wajasiliamali
hao wakiwa katika mafunzo ya ubanguaji bora wa korosho
Mkuu
wa Wilaya ya Lindi Shahibu Ndemangaakikabidhi cheti kwa mmoja wa wajasilimali hao.
No comments:
Post a Comment