Afisa mwandamizi wa Ubalozi wa Austria wenye makazi
yake Nairobi, Kenya. Bw. Kurt Muellauer akifungua Kongamano la Biashara
lililoandaliwa kwa ushirikiano kati ya Chama cha Wafanyabiashara, Wakulima na
Wenyeviwanda Tanzania (TCCIA) na Ubalozi wa Austria.
Kongamano hilo
nimwendelezo wa jitihada za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani ambao
unawakilisha pia nchini Austria na wadau mbalimbali katika kutekeleza
diplomasia ya uchumi.
Pamoja na mambo mengine kampuni 8 kati 16 zinatarajiwa
kufanya ziara jijini Dodoma tarehe 29 Januari kwa lengo la kukutana na Mawaziri
wa Kilimo; Nishati; Fedha na Mipango; Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wanawake na Watoto na Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Kongamano hilo
limefanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Uhamasishaji Uwekezaji wa TIC, Bw.
John Mnali, pamoja na wadau wengine wakimsikiliza kwa makini Bw.Muellauer
(hayupo pichani).
Baadhi ya wawekezaji kutoka Austria nao
wakifuatilia kongamano hilo.
Kaimu Rais wa Chama cha Wafanyabiashara, Wakulima
na Wenyeviwanda Tanzania (TCCIA), Bw. Octavian Mshiu, akizungumza katika
ufunguzi wa kongamano hilo, ambapo alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji
nchini na kuunga mkono Sera ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, ya Uchumi wa Viwanda nchini.
Afisa wa Uhamasishaji Uwekezaji (TIC), Bi. Diana
Ladislaus akizungumzia fursa za uwekezaji nchini wakati wa kongamano hilo.
Majadiliano yanayoonesha dalili ya kuzaa matunda ya
ushirikiano kati ya Wafanyabiashara wa Tanzania na Austria
No comments:
Post a Comment