Kamati ya fedha,utawala na mipango ya
halmashauri ya Chalinze Wilaya ya Bagamoyo imeanza ziara ya kukagua na kuona vyanzo vya
mapato vinavyotokana na madini ya kokoto katika makampuni ya Z&A, Lavender
Infrastructure, China Gold,Nyanza Road Works, Jiwe Project, Mhingara Company Ltd
na Grand tech.
Kamati hiyo imeanza kufanya ziara
hiyo kwa robo ya pili ya mwaka wa fedha 2018/2019, katika ziara hiyo wajumbe
wamehoji kutaka kujua makampuni ya uchimbaji madini yanalipa kodi ya huduma na
ushuru wa mapato yatokanayo na kokoto.
Kwa upande wake mwenyekiti wa
halmashauri ya Chalinze Mheshimiwa Said Omari Zikatimu na kamati ya fedha alitaka kujua
kama makampuni hayo yanalipa ushuru na kodi kwa mujibu wa sheria ya fedha namba
9 ya serikali za mitaa ya mwaka 1982.
"Lengo la halmashauri yetu ni
kukusanya mapato kwa zaidi ya asilimia 100 Ili kuvuka malengo ya bajeti yetu na
kuziba mianya yote ya ukwepaji kodi na shuru mbalimbali. " alisema Zikatimu.
Hata hivyo kamati ya fedha ilipokuwa
ikikagua shughuli za uchimbaji wa kokoto iliweza kubaini baadhi ya makampuni
kuendesha shughuli zake pasipo kuwa na nyaraka mbalimbali za kisheria kama
leseni ya kuchimba madini, leseni ya biashara na nyaraka zingine kwa mujibu wa
sheria.
Kamati ilipobaini mapungufu hayo
ilitoa maagizo kwa wamiliki wa kampuni hizo kuwasilisha nyaraka husika ofisi ya
mkurugenzi mtendaji wa Halamsahauri haraka iwezekanavyo vinginevyo hatua za kisheria
zitachukuliwa dhidi ya makampuni tajwa kwa kukiuka sheria za uwekezaji.
No comments:
Post a Comment