Rais
Mstaafu wa awamu ya nne ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na washiriki wa kongamano la kuazimisha miaka
55 toka kuanzishwa kwa Chuo Kikuu hicho mapema hii leo Chuo Kikuu jijini Dar es
Salaam.
Mhadhiri
wa Heshima Prof. Tade Aina toka nchini Nigeria akielezea hali ya vyuo vikuu vya
Afrika katika muktadha wa Kimataifa wakati wa kongamano la kuazimisha miaka 55
toka kuanzishwa kwa Chuo Kikuu hicho mapema hii leo Chuo Kikuu jijini Dar es
Salaam.
Baadhi
ya washiriki wa kongamano maalum la kuazimisha miaka 55 toka kuanzishwa kwa
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakimsikiliza kwa makini Mhadhiri wa Heshima Prof.
Tade Aina toka nchini Nigeria wakati akielezea hali ya vyuo vikuu vya Afrika
katika muktadha wa Kimataifa mapema hii leo Chuo Kikuu jijini Dar es Salaam.
Rais
Mstaafu wa awamu ya nne ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akifurahia jambo na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji
Joseph Sinde Warioba (kushoto) wakati wa kongamano la kuazimisha miaka 55 toka
kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mapema hii leo Chuoni hapo,
katikati ni Mhadhiri wa Heshima Prof. Tade Aina toka nchini Nigeria.
Rais
Mstaafu wa awamu ya nne ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam na Wakuu wa Vitivo wa Chuo hicho wakati wa kongamano la
kusherehekea kutimiza miaka 55 toka kuanzishwa kwa chuo hicho.
.......................................................
UONGOZI wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) takiwa kuhakikisha Chuo
hicho kinaendelea kuwa kiongozi miongoni mwa Vyuo Vikuu nchini.
Ushauri huo umetolewa na Rais mstaafu wa awamu ya Nne ambaye pia ni Mkuu
wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
alipokuwa akifungua maadhimisho ya miaka 55 ya chuo hicho leo Jijini Dar es
Salaam.
“Hiki ndicho Chuo kiongozi kati ya Vyuo Vikuu vyote hapa nchini,
mnatakiwa kuhakikisha kinaendelea kuwa kiongozi huku Vyuo vingine vikifuatia”.
Alisema Dkt. Kikwete.
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa
Lwekaza Mukandara amesema kuwa pamoja na changamoto zinazo kikabili chuo hicho
wanaishukuru Serikali kwa kuendelea kusaidia katika kuleta maendeleo ya chuo
hicho.
Alisema kuwa baadhi ya changamoto zimetatuliwa kwa pamoja kati ya
Serikali na wahisani ambapo alisema kuwa ujenzi wa kumbi mpya za mihadhara,
Maabara za Kisasa na jengo la malazi,pamoja na ujenzi wa hosteli za
wanafunzi unaoendelea katika Kampasi ya Julius K. Nyerere ambayo itakuwa na
uwezo wa kutumiwa na wanafunzi 4000 mara itakapo kamilika.
Akiwasilisha mada juu ya “hali ya Taaluma Barani Afrika katika Muktadha
wa Kimataifa” Mhadhiri wa Heshima kutoka nchini Nigeria, Profesa Tade
Aina amesema kuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ni moja kati ya Vyuo Vikuu
mahiri barani Afrika ambapo kimetoa mchango mkubwa kwa ukombozi wa nchi nyingi
za bara hili.
Aliongeza kuwa yeye binafsi ni mnufaika mkubwa wa UDSM kwani amekuwa na
ushirikiano mkubwa na baadhi ya wahadhiri kutoka chuo hicho katika masuala
mbalimbali ya taaluma.
Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wakati wa
uwasilishaji mada alisema kuwa kipindi Chuo hiki kinaanzishwa aina ya masomo
yaliyokuwa yanafundishwa chuoni hapo yalikuwa na muelekeo kuandaa wafanyakazi
wa Serikali kwa wakati huo.
Na kuongeza kuwa muelekeo wa aina ya masomo uliendelea kubadilika kadri
ya siku zilivyokwenda kutokana na mabadiliko ya teknolojia na uhitaji wa soko
la ajira.
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kinaadhimisha miaka 55 tangu kuanzishwa
kwake mnamo mwaka 1961 kikiwa ni tawi la Chuo Kikuu cha London, ambapo awali
kilianzia katika mtaa wa Lumumba kikiwa na wanafunzi 14 kabla ya kujengwa
mahali kilipo sasa katika eneo la Mlimani.
No comments:
Post a Comment