Mkurugenzi
Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk.Helen Kijo- Bisimba
(katikati), Mkurugenzi wa Uwezeshaji na Uwajibikaji, Imelda Urio (kulia)
na Mkurugenzi wa Utetezi na Maboresho wa LHRC, Anna Henga , wakionesha
jarida la kupinga adhabu ya kifo wakati wa uzindi wake Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Uwezeshaji na Uwajibikaji, Imelda Urio (kulia), akisisitiza
jambo kwenye mkutano huo, kusho ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk.Helen Kijo- Bisimba.
Wanahabari wakifuatilia mkutano huo.
..............................
KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimefungua kesi ya kikatiba
kuhusiana na ulinzi wa haki ya kuishi na urekebishwaji wa sheria ya kanuni ya
adhabu juu ya ulazima wa kutolewa kwa adhabu ya kifo katika makosa ya uhaini na
mauaji.
Kesi hiyo imefunguliwa dhidi ya mwanasheria mkuu wa serikali
wakitaka ufafanuzi zaidi juu ya adhabu ya kifo, wakibainisha kuwa adhabu
hiyo haimpi nafasi mtuhumiwa kujirekebisha bali ni ya kulipiza kisasi.
Kituo hicho kimesema endapo Tanzania itatekeleza hukumu ya kifo kwa
sasa inamaanisha watu wapatao 228 na zaidi watapoteza maisha yao huku
wengine 244 wanasubiria maamuzi ya rufaa zao.
Akizungumza wakati akitoa tamko la kupinga adhabu ya kifo Dar es
Salaam leo Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Hellen- Kijo Bisimba alisema hadi
mwaka 2015 jumla ya watu 472 walikuwa wamehukumiwa kunyongwa.
Alisema kituo kinaiomba serikali kurekebisha sheria ya kanuni ya adhabu
na sheria ya ugaidi yenye kutoa adhabu ya kifo kwa makosa ya mauaji, uhaini na
ugaidi.
Dk. Bisimba alisema kituo kina sababu za kupinga adhabu hiyo ya
kifo na hawafurahii watu kuua wengine na ndio maana hawapendi pia hata
muuaji auawe.
“Adhabu ya kifo ni vigumu kuhakikisha kuwainatekelezwa tu kwa wale
watu ambao huwezi kuirekebisha kwani mfumo wa utoaji haki huwa pia na mianya ya
makosa na hivyo maisha ya mtu yanaweza kupotea bure,” alisema Dk. Bisimba na
kuongeza kuwa hakuna ushahidi wowote kuwa adhabu hiyo inaweza kuzuia watu
wengine kutokutenda makosa kama hayo.
Alisema licha ya adhabu hiyo kutokutekelezwa nchini kwa takriban
miaka 22 , taaarifa zinaonesha kuwa watu 72 ambao walishawahi kunyongwa
kutokana na adhabu hiyo.
Hata hivyo aliiomba serikali kutengeneza utaratibu wa kuelimisha jamii
juu ya kuheshimu haki za binadamu hususani haki zakuishi na kuweka mazingira ya
kuiheshimu haki hiyo, pia ibadilishe sheria kwa kuondoa adhabu ya kifo na
kuweka adhabu mbadala kwenye makosa ya jinai na kwa wafungwa waliopo mfano vya
muda mrefu gerezani.
No comments:
Post a Comment