Tuesday, October 18, 2016

DC BAGAMOYO ABAINI WIZI KATIKA KUKUSANYA USHURU WA MKAA KATA YA MBWEWE.



Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaji Majidi Hemedi Mwanga amebaini  upotevu  wa  fedha katika makusanyo ya ushuru  eneo  la Voda  kijiji  cha  Mpaji  kata ya Mbwewe yanayokana na mauzo ya mkaa.

Mkuu huyo wa wilaya alifika  katika eneo hilo kwa  kushtukiza  na kudai  mashine ya kieletroniki kwaajili ya risiti ambapo mkatisha  ushuru kijiji hicho hakuwa nayo.

Baada ya kukosekana  mashine ya kukusanyia ushuru mkuu wa wilaya  alidai  apatiwe  kitabu cha risiti za mkono zinazotolewa baada ya muuzaji  kulipia ushuru wa serikali ambapo kitabu  hic ho  kilionyesha kuanzia saa 12  asubui  mpaka saa 12  jioni  muda aliofika mkuu wa wilaya kitabu hicho kinaonyesha ushuru uliokusanywa ni wa Gunia  mbili tu sawa na shilingi elfu  mbili tu.

Kufuatia hali hiyo mkuu wa wilaya ameamuru mkusanya ushuru aliyeteuliwa na kijiji hicho kuchukuliwa na polisi kwaajili ya mahojiano ilikuelezea mfumo anatumia kutunza  kumbukumbu mara anapokusanya ushuru.

Mkuu wa wilaya Majidi Mwanga amelazimika kuweka kambi  katika kijiji hicho usiku mzima  ili kubaini  namna wakusanyaji ushuru huo wanavyoiba fedha za serikali kwa manufaa yao.

Wafanyabiashara wa mkaa eneo la Voda kata ya Mbwewe wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Hemedi  Mwanga.



Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majidi Mwanga akizungumza na wafanyabisahara wa mkaa eneo la Voda kijiji cha  Mpaji kata ya  Mbwewe




Gari  hili limebeba magunia kadhaa ya mkaa huku ushuru ukionyesha gunia 2 tu



Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majidi Mwanga akiwa katika eneo la wauza mkaa kiji cha Mpaji kata ya Mbwewe.

No comments:

Post a Comment