Kulia ni Naibu katibu mkuu wa umoja wa wanazuoniwa kiislamu tanzania,
Sheikh Muhammad Issa, na kushoto ni mkurugenzi wa Benkiya Amana, Dkt. Muhsini
Masoud wakifungua pazia ikiwa ni ishara ya kuzindua rasmi huduma ya zaka katika
Benki ya Amana.
............................................
Benki ya Amana imezindua huduma mpya ya kukusanya
na kugawa zaka ili kuwarahishia wateja wake kuweza kutekeleza ibada ya Zaka
ambayo ni nguzo ya tatu katika uislamu, lakini piya utekelezaji wake ni amri
kutoka kwa Mwenyezimungu Subhaanahu Wataala.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa
Benki ya Amana Dkt. Muhsini Masoudi amesema Benki inayofuata misingi ya
kiislamu inapaswa kufanya shughuli zake kwa uwazi na uadilifu ili kujenga
uaminifu kwa wateja wake.
Alisema hudumua hiyo mpya katika Benki hiyo inayofuata
sheria ya uislamu itamuwezesha mteja kufanya hesabu ya kiasi anachotakiwa
kutoa zaka ambapo benki hiyo kupitia
Bodi ya Sharia itasimamia namna ya
kugawa zaka hiyo kwa makundi yanayohusika kwa mujibu wa
mafundisho ya uislamu.
Aidha, alisema kufuatia huduma hiyo tovuti ya
Benki ya Amana imeweka sehemu ya kufanyia hesabu kuhusu kiwango kinachotakiwa kulipiwa zaka kwa
kuingia kwenye (www.amanabank.co.tz/sw/akaunti-ya-akiba-binafsi-zakat-service).
Alisema
katika kufanikisha huduma hiyo,
Benki ya Amana itafungua akaunti maalum
ya zaka na kwamba mara baada ya kuikusanya itagaiwa kwa watu maalum
wanaostahiki kupewa kama itakavyoamuliwa na chombo maalum cha kugawa zaka
ambacho kitakuwa na wajumbe kutoka Benkiya Amana, Bodi ya Sharia na uwakilishi
kutoka kwenye jamii.
Katika kuwatoa wasiwasi wateja wake kuhusu huduma
hiyo ya Zaka, Mkurugenzi wa Benki ya Amana Dkt. Muhsini Masoud alisema katika
kutekeleza hilo kwa ufanisi,kutakuwa na ukaguzi wa ndani, ukaguzi wa nje pamoja
na ukaguzi kutoka Benki kuu ili kuona ni
kiasi ganicha pesa kimeingia
kwenyeakaunti zaka na mgawanyo wake.
Aliongeza kwa kusema kuwa, huduma hiyo ya zaka kwenye
Benki ya Amana itawahusu waislamu tu kwakuwa hilo ni jambo la ibada na wateja
wasiokuwa waislamu hawataingia kwenye huduma hiyo na badala yake wataendelea
kupata huduma zingine kama kawaida.
Kwa upande wake mjumbe Bodi ya Sharia katika
Benki hiyo Dkt. Abdallaah Tego alisema tatizo lililopo katika jamii ni uaminifu
na ni taasisi gani ambayo inaweza
kusimamia zaka jambo ambalo limekuwa
kikwazo kwa wenye kutaka kutoa zaka.
Alisema Benki ya Amana kwa kuanzisha huduma ya
zaka itapelekea waislamu wengi
kutekeleza ibada hiyo ya zaka kwakuwa Benki ni chombo chenye dhamana
hali inayopelekea kutokuwa na wasiwasi nayo katika ukusanyaji na ugawaji wa zaka.
Dkt. Tego alisema lengola zaka ni kuondoa
umasikini kwenye jamii kwa kuangalia
makundi yaliyokusudiwa na kwa namna gani
wanaweza kupata mgao wa zaka ili kuondoa tofauti kubwa iliyopo kati ya
matajiri na masikini.
Nae naibu katibu mkuu wa Umoja wa wanazuoni wa
kiislamu, sheikh Muhammad Issa alisema
zakani swala la kijamii hivyo itakavyotekelezwakwa ukamilifu wake faida
itarudi kwenye jamii na hilo ndilo lengo
lazaka.
Alisema zaka ni nguzo ya tatu katika nguzo za
kiislamu na kwamba utekelezaji ni amri kutoka kwa Mwenyezimungu Subhaanahu
Wataala lakini bado utekelezaji wake upo katika kiwango kidogo.
Ameongeza kwa kusema kuwa kuanzishwa kwa huduma
ya zaka katika Benki hiyo itasaidia
waislamu wengi kupata hamasa ya
kuisimamisha nguzo hiyo ya tatu ya uislamu.
Aidha, alisema jamii inahitaji huduma mbalimbali
ambapo zaka ikitolewa na kugawanywa katika makundiyake itasaidia katika huduma
za kijamii.
Mkurugenzi
wabenkiya Amana, Dkt. Muhsin Masoud akizungumza wakatiwa uzinduzi huo
maka makuu ya Benki hiyo jijini Dar es Salaam
Mjumbe wa Bodi ya sharia katika Benki ya Amana,
Dkt. Abdallaah Tego akizungumza katika uzinduzi huo.
Sheikh Muhammad Issa akizungumza katika uzinduzi
huo
Kushoto ni Mkrugenzi wa Benki ya Amana, Dkt.
Muhsin Masoud akizungu mza na waandishi wa habarikatika uzinduzi huo, kulia ni
naibu katibu mkuu wa Umoja wa wanazuoni
wa kiislamu Tanzania, Sheikh Muhammad Issa.
No comments:
Post a Comment