TAKUKURU MKOA WA PWANI YAFANIKIWA KUOKOA ML.29 KUTOKA KWA WAKUSANYA USHURU WILAYA YA MAFIA

 

TAKUKURU MKOA WA PWANI YAFANIKIWA KUOKOA ML.29 KUTOKA KWA WAKUSANYA USHURU WILAYA YA  MAFIA



Na Victor Masangu,Pwani


Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rusha Takukuru Mkoa wa Pwani imefanikiwa kudhibiti na kuokoa kiasi cha  zaidi ya shilingi milioni 29 katika Halmashauri ya  Wilaya ya Mafia ambazo zilikuwa mikononi mwa wakusanyaji wa ushuru kinyume kabisa na taratibu.


 

Hayo yamebainisha na Naibu mkuu wa Takukuru Mkoa wa Pwani Ezekia Sinkala wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na utekelezaji wa kazi na majukumu mbali mbali  ambayo imeyafanya kwa kipindi cha kuanzia Aprili hadi Septemba mwaka 2026.


Naibu mkuu huyo amebainisha kwamba fedha hizo zimefanikiwa kuokolewa kutoka  katika Wilaya ya Mafia ambazo zilikuwa fedha za makusanyo  ya mapato kwa mfumo wa njia ya mashine(POS).


"Kutokana na kuwepo kwa fedha hizo za umma katika akaunti ya Imprest kwa kufuatilia ukusanyaji wa mapato na uwekaji wa fedha  hizo benki ndio Takukuru tulipoingilia kati na kubaini kiasi hicho kuwa katika mikononi mwa wakusanyaji bila kuweka benki,"amebainisha Naibu huyo.


Aidha Takukuru Mkoa wa Pwani imefanikiwa kuokoa kiasi cha shilingi milioni moja ambazo zilitolewa na wananchi wa kijjji cha Nyamwage Wilaya ya Rufiji kwa ajili ya kumpatia mtumishi wa Ruwasa ili waunganishiwe maji kinyemela.


Pia Takukuru katika kutekeleza majukumu yake imefanikiwa kuokoa vifaa mbali mbali vya ujenzi vyenye thamani na kiasi cha shilingi laki nane katika kituo maalumu cha Ikwiriri Wilaya ya Rufiji fedha ambazo zilitakiwa kutekeleza mradi wa ujenzi wa darasa katika shule ya msingi shikizi ya Nyamitumba.


Katika hatua nyingine Takukuru Mkoa wa Pwani imefanikiwa kufikisha elimu ya masuala ya rushwa kwa jamii kwa  wananchi wapatao elfu 27 kutoka maeneo mbali mbali.


Pia Takukuru imetoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano ikiwemo kufika kwa ajili ya kuweza kutoa ushahidi katika mahakama kwa kesi ambazo zinaendelea za makosa ya rushwa zilizofanyiwa uchunguzi.

Comments

Popular posts from this blog

MATOKEA DARASA LA SABA 2018 HAYA HAPA.

MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR AUNGURUMA PWANI ASEMA DHAMIRA KUBWA YA CCM NI KUWAHUDUMIA WANANCHI

HAYA HAPA MATOKEO YA DARASA LA SABA 2017.

MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2016 HAYA HAPA