Monday, October 24, 2016

WAZIRI WA AFYA WA EQUITORIAL GUINEA AFANYA ZIARA HAPA NCHINI ATEMBELEA KITUO CHA UTAFITI WA MARALIA BAGAMOYO.

Waziri wa Afya wa Equitoria Guinea Salomon Ingema, akisalimiana na katibu tawala wa wilaya ya Bagamoyo, Erica Yegella wakati alipowasili katika kituo cha utafiti cha Ifakara Health Center Bagamoyo
Waziri wa Afya wa Equitoria Guinea Salomon Ingema, akisalimiana na Mkurugenzi wa Ifakara Health Institute (ihi) Prof. Hounorati Masanja, mara baada ya kuwasili katika kituo hicho cha utafiti mjini Bagamoyo, ambapo waziri huyo amekuja kujifunza mambo mbalimbali kuhusu utafiti wa magonjwa ikiwemo  malaria.
...............................................

Serikali za nchi za Afrika zimeombwa kuwekeza katika Taasisi za utafiti ili kukabiliana na tatizo la fedha katika kufanya tafiti za chanjo na dawa kwaajili ya magonjwa mbalimbali.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Afya ya Ifakara (ihi) Prof. Hounorati Masanja alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumpokea waziri wa Afya wa Equitorial Guinea ambae aliitembelea Taasisi hiyo.

Pro. Masanja amesema kwa sasa taasisi hiyo inakabiliwa na changamoto ya fedha ambapo inawachukua muda mrefu kufikia malengo ukilinganisha na msukumo wa ushindani ulipokatika nchi zilizoendelea.

Kwa upande wake mkuu wa mradi wa utafiti un ashirikiana kati ya Tanzania na Equitorial Guinea, Prof. Salim Abdullah, alisema ujio wa waziri huyo hapa nchini ni kujifunza mambo mbalimbali kuhusu utafiti ili kuimarisha vituo vyao vilivyopo katika nchi yao.

Alisema wamekuwa wakishirikiana na nchi hiyo ya Equitorial Guinea kwa zaidi ya miaka miatatu sasa ambapo safari ya waziri huyo hapa nchini itaimarisha uhusiano uliopo baina ya nchi hizo mbili hasa katika utafiti na Afya kwa ujumla.

Awali akifungua mkutano wa kumkaribisha waziri huyo, Katibu tawala wilaya ya Bagamoyo, bi Erica Yegella, alisema Tanzania inakabiliwa na ugonjwa wa malaria hasa kwa watoto walio chini ya umri miaka mitano na kina mama wajawazito.

Alisema serikali inajitahidi kukabiliana na tatizo la malaria katika mambo mbalimbali ikiwemo kuthamini kazi zinazofanywa na wataalmu wa utafiti ili kuweza kupata matokeo mazuri.

Aidha, Katibu tawala huyoalimshukur waziri huyo wa Afya kwa kutembelea Bagamoyo kwani ziara hiyo itadumishi ushirikiano ulipo na kubadilishana uzoefu.      
 
Kwa upande wake waziri wa Afya wa Equitorial Geinea, Solomon Ingema, alisema ugonjwa wa Malaria ni tatizo linalosumbua katika nchi za Afrika na kwamba sisi katika nchi yetu tunahitaji kuwekeza katika utaalamu wa utafiti ili  kukabiliana natatizo  hili ambalo mara nyingi huwasumbua watoto wadogo.


Alisema, nchi yetu ya Equitorial Guinea ni ndogo sana ina idadi ya watu milioni moja na laki mbili tu hivyo tuna kila sababu ya kujiimarisha kitaaluma ili watu wetu wasipate malaria ambapo tutafanikiwa  kwa  kujifunza kutoka  kwa watu  wazoefu  kama Tanzania.

Kwa zaidi ya miaka mitatu sasa imekuwa ikishirikiana na Tanzania katika kufanya utafiti kuhusu chanjo ya malaria na tiba hali iliyomvutia waziri huyo wa Afya kutembelea Tanzania.
  
Waziri wa Afya wa Equitoria Guinea Salomon Ingema, akisaini kitabu cha wageni kabla ya kuanza kwa kikao na wenyeji wake.

Wafanyakazi wa Ifakara Health institute wakifuatilia mazungumzo ya waziri wa Afya wa Equitoria Guinea Salomon Ingema.


Wafanyakazi wa Ifakara Health institute wakifuatilia mazungumzo ya waziri wa Afya wa Equitoria Guinea Salomon Ingema.


Kushoto ni mkuu wa Mradi wa utafiti Prof. Salim Abdulla.
Katibu tawala wilaya ya Bagamoyo Erica Yegella akifungua kikao hicho.

Kushoto ni kaimu Mganga  mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Dkt. Tumaini Baion.

Kamati ya ulinzi na usalamawilaya, ikiwa makini  kufuatilia mazungumzo hayo.
Mkuu wa mradi, Prof. Salim Abdulla akitoa historia fupi ya kituo cha Ifakara Health Institute.

Waziri wa Afya wa Equitoria Guinea Salomon Ingema akipata maelkezo kutoka kwa  mtaalam wa (ihi)

Waziri wa Afya wa Equitoria Guinea Salomon Ingema akiwa katika picha ya pamoja na wenyeji wake.

No comments:

Post a Comment