JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI TAREHE 11-10-2016.
JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALIYEJULIKANA KWA
JINA LA PAUL JONES KINA, MIAKA 34, MZANAKI, MWENDESHA PIKIPIKI (BODABODA) MKAZI
WA MTAA WA KANYERERE KWA TUHUMA ZA KUMBAKA
MTOTO WAKE WA KUMZAA JINA LINAHIFADHIWA, MWENYE UMRI WA MIAKA 10, MWANAFUNZI WA
DARASA LA NNE SHULE YA MSINGI TAMBUKA RELI.
TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 01.10.2016 MAJIRA YA SAA 23:00HRS KATIKA MTAA WA KANYERERE KATA YA
BUTIMBA WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, BAADA YA KUPATIKANA KWA TAARIFA
KUTOKA KWA RAIA WEMA.
INADAIWA KUWA MTUHUMIWA TAJWA HAPO JUU ALIKUWA NA KAWAIDA (TABIA) YA
KUMBAKA BINTI YAKE KWA MUDA MREFU, NDIPO WATU WAKARIBU MAJIRANI WALIWEZA KUTOA
TAARIFA POLISI KUHUSIANA NA KITENDO HICHO, AIDHA BINTI ALIWEZA KUPELEKWA
HOSPITALI KWA AJILI YA UCHUNGUZI NDIPO IKATHIBITIKA KWAMBA NI KWELI AMEBAKWA.
MTUHUMIWA WA KITENDO HICHO CHA UBAKAJI AMEKAMATWA YUPO NDANI, TAYARI
JALADA LAKE LA MASHITAKA LIMEPELEKWA KWA MWANASHERIA WA SERIKALI, HIVYO MUDA
WOWOTE KUANZIA HIVI SASA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI, ILI HATUA ZA KISHERIA ZIWEZE
KUCHUKULIWA DHIDI YAKE.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI
ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA, AKIWATAKA WATU WOTE WENYE
KESI ZA AINA KAMA HIYO ZA KUBAKWA AU UNYANYASAJI WA KIJINSIA KUTOA USHIRIKIANO
KWA JESHI LA POLISI NA MAHAKAMA.
AIDHA, AMEWAKUMBUSHA MASHAHIDI WA KESI ZA
AINA KAMA HII KUACHA TABIA YA KUMALIZANA KIENYEJI NYUMBANI HADI KUPELEKEA KESI
NYINGI KUHARIBIKA BALI MASHAHIDI WANATAKIWA WAKATOE USHAHIDI MAHAKAMANI ILI
HAKI IWEZE KUPATIKANA.
IMETOLEWA NA:
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA
No comments:
Post a Comment