Naibu
Waziri Ofisi ya Rais , Tawala za mikoa na serikali za mitaa (Tamisemi),
Selemani Jafo, akipewa maelekezo juu ya matumizi ya mfumo wa kukusanyia mapato.
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais , Tawala za mikoa na serikali za mitaa (Tamisemi),
Selemani Jafo, akiwa na mbunge wa Nzega Hussein Bashe katika ukaguzi wa bweni
la wasichana wilaya ya Nzega.
.........................
KUTOKANA na baadhi ya wananchi kuwafanyia vitendo vya ushirikina
watumishi katika Halmashauri mbalimbali nchini, Naibu Waziri Ofisi ya Rais ,
Tawala za mikoa na serikali za mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo ameonyesha
kukerwa na tabia hiyo inayowasababishia watumishi kupata msongo wa mawazo na
wengine kuomba kuhamishwa vituo vyao vya kazi.
Jafo alitoa kauli hiyo alipokuwa akikagua zahanati mpya iliyopo kijiji
cha Ziba katika Jimbo la Manonga wilayani Igunga mkoani Tabora na alipokuwa
akizungumza na watumishi wa wilaya hiyo.
Alimuagiza mkuu wa wilaya ya Igunga kutenga muda yeye na kamati yake ya
ulinzi na usalama kuwafikishia ujumbe wananchi wa wilaya ya Igunga kuwakemea
wenzao wenye tabia hiyo wilayani humo ili kuacha tabia hiyo ovu.
Naibu waziri Jafo alisisitiza kwamba tabia hiyo imewasababishia
baadhi ya watumishi walio tendewa vitendo hivyo kupatwa na msongo wa mawazo na
kuomba kuhama maeneo walio pangiwa.
Naibu Waziri alisema kwamba jamii inapaswa kuwathamini watumishi kwani
wametoka maeneo mbalimbali ya nchi ili kuja kuwatumikia wao hivyo wanatakiwa
kuwathamini na kuwaheshimu kwa kulinda utu wao.
” Watani zangu mliopo hapa
Wasukuma na Wanyamwezi mmepata zahanati nzuri naomba muitunze. Pia sitaki
kusikia daktari au mhudumu amelala asubuhi anajikuta ng’ambo ya barabara
au katika kiwanja cha mpira,”alisema Jafo.
Aidha, alikemea kitendo cha sungusungu walio mchapa viboko mwalimu mkoani
humo huku akiwaagiza wakuu wa wilaya maeneo yote kupambana na tabia za
udhalilishaji wanazo fanyiwa watumishi wa umma katika jamii ili waweze kufanya
kazi kwa amani na kujiamini.
Aliwapongeza viongozi wa mkoa wa Tabora kwa umoja na ushirikiano wao
katika kuwaletea maendeleo wananchi wa mkoa huo.
No comments:
Post a Comment