Uongozi wa Hospitali ya Taifa
Muhimbili unapenda kuutarifu Umma kwamba haijamzuia Bi. Mwajuma Ramadhani
Kimweri kutoka hospitalini kwa madai ya kushindwa kulipa pesa za matibabu kama
ilivyoandikwa na Gazeti la Jambo Leo lenye namba ISSN 7826 No 2589, hivyo
taarifa hizo si za kweli.
Katika ukurasa wa mbele, gazeti hilo limechapisha taarifa yenye kichwa
cha habari kinachosema “Mgonjwa saratani azuiwa Muhimbili miezi miwili ni baada
ya kushindwa kulipa deni la Sh. 330,000”.
Bi. Mwajuma Ramadhani Kimweri kwa mara ya kwanza alilazwa Muhimbili
Agosti 29, 2016 akitokea mkoani Morogoro na kuruhusiwa Septemba 10, 2016
na Septemba 23, 2016 alilazwa tena na kuruhusiwa Septemba 24,
2016.
Baada ya vipimo vya awali kufanyika Septemba 29, 2016 alilazwa tena na
kufanyiwa upasuaji Septemba 30, 2016 na kuruhusiwa Oktoba 04, 2016 baada
ya taratibu za matibabu kukamilika.
Mgonjwa aliingizwa kwenye utaratibu wa msamaha na kuchangia
Shilingi 70,000 tu, kati ya Shilingi 400,142.33. Hivyo si kweli kwamba
mgonjwa alilipa Shilinngi 380,000 kama ilivyoandikwa na gazeti hilo.
Kuhusu tiba ya mionzi, Bi. Mwajuma Ramadhani Kimweri amefanyiwa vipimo
vingine hivyo atatakiwa kurejea baada ya wiki tatu kwa ajili ya majibu na si
kweli kwamba Muhimbili imezuia uhamisho wake kwenda Taasisi ya Saratani ya
Ocean Road kwa ajili ya tiba hiyo.
Imetolewa na;
Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili
Oktoba 10, 2016.
No comments:
Post a Comment