Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Kamishna msaidizi wa Polisi, ACP- Boniventure Mushongi.
......................................................
Jeshi la
Polisi mkoani Pwani linamshikila mwalimu
wa madrasa kwa tuhuma za kuendesha mafunzo ya
kihalifu katika madrasa yake.
Akitoa Taarifa kwa vyombo vya Habari kamanda wa
Polisi Mkoawa Pwani, Kamishna msaidizi wa Polisi, ACP-Boniveture Mushongi alisema
mwalimu huyo amekamatwa kutoka na
taarifa walizopata kutoka raia wema ambao walikuwa na mashaka kuhusu mwenendo
wake.
Kamanda Mushongi alisema mwalimu huyo
mwanamke Ashura Saidi mwenye umri wa
miaka 47, ni mwalimu wa madrsa ijulikanayo kwa jina la ARAHMA, iliyopo eneo
la Kimarang'ombe kata ya Nianjema Tarafa ya Mwambao wilayani Bagamoyo
alikamatwa kufuatia msako wa kushtukiza
uliofanywa na makachero majira ya saa 9 za jioni siku ya tarehe 01
Oktoba 2016.
Kamanda Mushongi aliongeza kuwa katika upekuzi
mtuhumiwa alikutwa na bomu la moshi lenye namba G2020c.SS-ATCS
lililokutwa kwenye makazi yake.
Aliongeza kuwa katika uchunguzi wa awali umebaini
madrasa hiyo inamilikiwa na taasisi ya AKHA LAAGUL ISLAM ambayo ilisajiliwa kwa
lengo la kulelea watoto yatima.
Kituo hicho kimekuwa kikitoa huduma kwa watoto
kutoka sehemu mbalimbali ikiwemo Dar es Salaam, Handeni Tanga, Mlandizi, na
Bagamoyo mkoani Pwani.
Aidha, Kamanda Mushongi alisema kuwa
pamoja na kumshikilia mwalimu huyo wa Madrasa, polisi inawashikilia
watoto 22 waliokuwa katika kituo hicho am bao 16 kati yao ni wasichana na 6 ni
wavulana.
No comments:
Post a Comment