Mkuu
wa wilaya ya Kongwa Mh Deo Ndejembi akizindua kampeni ya kuondoa Njaa wilaya ya
Kongwa, (ONJAKO)
Mkuu
wa wilaya ya Kongwa Mh Deo Ndejembi akizungumza mara baada ya kuzindua kampeni
ya kuondoa Njaa wilaya ya Kongwa, (ONJAKO)
...........................................
Mkuu wa
Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma Mhe Deo Ndejembi ameanzisha kampeni ya kuondoa
Njaa wilaya ya Kongwa, (ONJAKO) yenye dhamira ya kuwasaidia wananchi kuondokana
na hali yanjaa ambayo ni kadhia kubwa katika maeneo mbalimbali ya Wilaya hiyo
sambamba na Taifa kwa ujumla.
Kuanzishwa
kwa Kampeni ya Okoa njaa Wilaya ya Kongwa imejili wakati Mkuu huyo wa Wilaya ya
Kongwa Akizungumza na Wakuuwa Idara na vitengo, Madiwani wa Kata zote zilizopo
Wilayani humo, Watendaji wa Kata, Maafisa Tarafa, Waratibu Elimu Kata,
Wenyeviti wa Vijiji vyote 87 vya Wilaya ya Kongwa na watendaji wao, pamoja na
wadau waalikwa na Kilimo.
Akizindua
kampeni hiyo Dc Ndejembi alisema kuwa Kampeni hiyo imezinduliwa Mwezi Octoba
kwa ajili ya msimu wa mwaka 2016/2017 na inatarajiwa kuwa kampeni Endelevu
katika kipindi cha Miaka mitano.
Ameeleza kuwa huu ni mkakati maalumu katika Wilaya ya Kongwa Mkoani
Dodoma ili kukabiliana na hali ya Ukame ambayo ni tatizo sugu katika maeneo
mengi nchini.
Kutokana na hayo DC Ndejembi ameagiza kuwa na kilimo
cha Mtama zaidi kuliko Mahindi. Kwani Wilaya ya Kongwa ina Kaya 59141, na kila
kaya kama ikilima Heka mbili (2) za Mtama, Mavuno itakuwa Tani 71000, za Mtama
sawa na 83% ya hitaji la chakula Wilayani Kongwa.
Katika kukabiliana na njaa mahitaji mengine mahususi
yametajwa ikiwa ni pamoja na Kuongeza uzalishaji wa mtama toka tani 1/ Hekta
mwaka 2016 hadi tani3/hekta ifikapo mwezi June 2021, Kuongeza Uzalishaji wa
Muhogo mbichi toka tani 6/hekta Mwaka 2016 hadi tani 10 hekta mwaka 2029,
Kuongeza uzalishaji wa zao la Alizeti toka tani 1.2/ hekta mwaka 2016 hadi tani
1.8/hekta mwaka 2021.
Pia Mhe Ndejembi alisema kuwa mahitaji mengine ni
pamoja na Kuongeza uzalishaji wa ufuta toka tani 0.5/hekta mwaka 2016 hadi tani
1.2/hekta ifikapo june 2021, pamoja na Kuongeza pato la Mtu/watu toka Tsh
500,000/= Mwaka 2016 hadi Tsh 800,000/= June 2021.
DC Ndejembi ameagiza kufanyika utaratibu wa
kuhakikisha kila kaya inalima Heka zisizopungua mbili (2) za Mtama, Mbili za
Mahindi, kulingana na eneo husika wakishauriwa na maafisa ugani lakini mtama ni
lazima kwa kila kaya hata kama analima mahindi.
Pia amewaagiza vijana wote wasio na kazi Wilayani
Kongwa wapewe Hekari mbili kila mmoja ili waache kucheza pool table na
kujihusisha na vikundi Ovu vya wizi na matumizi ya Dawa za kulevya.
Saambamba na hayo Mhe Ndejembi aamepiga marufuku
kuchezwa mchezo wa Pool Table mpaka ifikapo majira ya saa 10 jioni, hivyo kwa
yeyote atakaye kiuka utaratibu huo atakuwa amekiuka amri halali ya serikali.
No comments:
Post a Comment