Monday, October 24, 2016

GARI ILIYOIBWA DARES SALAAM YAPATIKANA KIWANGWA BAGAMOYO.




Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani kamishna msaidizi wa Polisi, Boniventure Mushongi akiwaonyesha waandishi wa habari gari lililoibwa na kupatikana, katika kituo cha Polisi Bagamoyoleo Tarehe 24/10/2016, kushoto ni mmiliki wa gari hilo  Kapteni Innocent Philip Dallu.
..................................

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANI
https://pbs.twimg.com/profile_images/378800000627599404/78e46699bdd17a7a394badc02f2b2a58.png
 
TAAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

Jeshi la Polisi Mkoa wa  Pwani tumefanikiwa kulipata Gari lililoibiwa jana eneo la Mbezi juu jijini Dar es Salaam majira ya saa 12:00 mchana lenye namba T.400 DEH aina ya Toyota Harier mali ya afisa wa jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kapteni Innocent Philip Dallu.

Gari hilo lilikamatwa kwenye kizuizi cha Barabarani kilichokuwa kimewekwa na askari katika barabara ya Msata /Bagamoyo katika eneo  la Bago kata ya Kiwangwa  wilaya ya Bagamoyo majira ya saa 00: 40 usiku wa kumakia leo.

Katika tukio hilo Jeshi  la  Polisi mkoa wa Pwani tunamshikilia  Ezekiel Daud 25  mfanyabiashara  mkazi wa  mkoa  wa Kilimanjaro na  tunaendelea na msako  wa kumtafuta  dereva aliyekuwa  akiendesha gari  hilo Joshua Elia  Adam  mwenye leseni namba  4001944688  ambae  alitoroka.

Mtuhumiwa  huyo tunamkabidhi kwa wenzetu  wa mkoa wa kipolisi Kinondoni  kwaajili ya taratibu  zingine  za kisheria.

Imetolewa na
Boniventure Mushongi-ACP
Kamanda wa Polisi (M) Pwani
Tarehe 24/10/2016. 


Kamanda wa polisi mkoa wa pwani Kamishna msaidizi wa Polisi, ACP- Boniventure Mushongi akitoa Taarifa kwa waandishi wa habari Bagamoyo leo Tarehe  24/10/2016.


Mmiliki waGari hilo  Kapteni Kapteni Innocent Philip Dallu, akizungumza na waandishi wa habari katika kituo cha Polisi Bagamoyo leo Tarehe 24/10/2016.

No comments:

Post a Comment