Thursday, October 6, 2016

MAHAFALI SIRAJUL MUNIR PRIMARY SCHOOL BAGAMOYO YALIKUWA HIVI.


Mwalimu Omari  Kisina akiongoza skauti kwa  lugha ya kiarabu.



Mgeni rasmi  Afisa rasilimali watu The Islamic Foundation, (TIF) Musa Buluki akizungumza katika mahafali hayo,  ambae alimuwakilisha Mwenyekiti wa wa TIF Aref Nahd
 

Amiri wa taasisi ya Sirajul Munir Islamic Center (SIMIC) Ustadhi, Abdallaah Kindamba akizungumza katika mahafali hayo.
....................................... 
Mwenyekiti waTheIslamic Foundation Al akhi Aref Nahdi, amewataka wazazi na walezi ncchini  kuwapa watoto wao elimu ya dini ili kuwajengea  misngi mizurii ya maisha ya duniani na akhera.

Akitoa nasaha hizo kwa niaba ya Mwenyekiti waThe Islamic Foundation ambae ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika mahafali ya shule ya SirajulMunir Bagamoyo, Afisa rasilimali watu wa The Islamic Foundation  Musa Buluki, alisema elimuya dini ndiyo msingi wa maisha ya binadamu katika kuwa namaadili mema  na kutekeleza uadilifu  katika majukumu yake ya kila siku.

Alisema Mwenye elimu ya dini anafanya kazi kwa kuchunga haki za watu mbalimbli, uadilifu na kutenda haki huku akijiepusha na mambo ya haramu kama vile rushwa na kuwafanyia watu dhulma katika kazi zake.

Aliongeza kwa kuwaasa wazazi kuhakikisha wanawasimamia watoto wao wanaomaliza katika shule za kiislamu kuwajengea misingi mizuri ya kuendelea na masomo yao ili wasipoteze kile  maadili mema waliyopata katika katika shule za kiislamu.

Akiendelea kuzungumza kwa niaba ya mwenyekiti wa TIF, Buluki aliwakumbusha wazazi kulipa ada kwa wakati katika shule zinazomilikiwa na waislamu kwakuwa katika kufanya hivyo wanapata faida ya kuwapa  elimu watoto wao, lakini pia ni sehemu ya kuchangia maendeleo ya uislamu katika harakati za kuendeleza elimu kwa jamii.

Alisema ada zinazotolewa husaidia uendeshaji wa shule ikiwemo malipo ya mishahara ya walimu, na vitendea kazi  na  kwamba changamoto mbalimbali zinazozikabili shule za kiislamu zinatatuliwa na viongozi katika mazingira magumu ili jamii ya kiislamu iendelee kupata elimu iliyokuwa sahihi na yenye manufaa.

Aidha, Buluki alipokea changamoto zilizosomwa na uongozi wa shule ya SirajulMunir na kuahidi kuzifikisha  ofisini  kwaajili ya  kuangalia uwezekano wa kuzitatua kadiri itakavyowezekana.

Kwa upande wake Amiri wa Taasisi ya  SirajulMunir Islamic Center (SIMIC) Abdallaah  Kindamba, ambao ndiyo wamiliki wa shule hiyo amesema  wanaishukuru Taasisi The Islamic Foundation (TIF)  kwa ushirikiano wake katika mambo mbalimbali kwa Sirajulmunir hali inayoashiria mapenzi  na  moyo  wa  kujitolea  kwa viongozi wa  TIF jambo  ambalo  linapaswa kuigwa na taasisi zingine  katika  kushirikiana baina   ya taasisi  za  kiislamu.

Awali akisoma risala mbele ya mgeni rasmi mwalimu wa Taaluma wa Sirajulmunir, Masudi Kaihula alisema shule hiyo inakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo  kukosekana kwa ukuta wa shule hali inayopelekea usalama mdogo kwa mali za shule, upungufu wa vyumba vinne vya madarasa, maabara moja na maktaba ambapo alisema hali hiyo inatokana na shule hiyo inaendeshwa kwa ada za wanafunzi tu na kwamba shule inaendeshwa bila ya faida.

Aidha, katika risala hiyo mwalimu kaihula aliipongezaTIF kwa mchango wake kwa shule hiyo ambapo alisema TIF waliweza kujenga  vyumba vinne vya madarasa, ofisi nne, vyoo, msikiti  pamoja na visima viwili vya maji ambapo alisema kuwa, pamoja na juhudi hizo zilizofanywa na  TIF bado shule hiyo inahitaji msaada zaidi ili kufanikisha malengo yake katika kuboresha mazingira ya shule.

Shule ya SirajulMunir ilianza mwaka 2004 ikiwa na wanafunzi kumi na nane tu ambamo mpaka sasa inawanafunzi 303 na kwamba tayari shule hiyo imetoa wahitimu wa darasa la sita kwa  miaka sita sita sasa.
Kulia ni Mgeni rasmi katika mahafali hayo, Afisa rasilimali watu wa The Islamic Foundation, Musa Buluki ambae alimuwakilisha Mwenyekiti wa The Islamic Foundation, Areef Nahdi, kushoto ni Amiri wa taasisi ya SirajulMunir Islamic Center ambao ndio wamiliki wa shule hiyo.


Baadhi ya wahitimu wa darasa la saba wa shule ya msingi ya SirajulMunir iliyopo kata ya Nianjema wilayani  Bagamoyo wakifuatilia  kinachoendelea katika mahafali hayo.



Baadhi ya wazazi waliohudhuria katika mahafali hayo pamoja na famila zao.


Wanafunzi wa shule ya Msingi ya Sirajulmunir iliyopo Nianjema wilayani Bagamoyo wakionesha michezo mbalimbali.
Wahitimu wa darasa la saba shule ya msingi SirajulMunir iliyopo Nianjema wilayani Bagamoyo wakisoma Qur ani na kuitafsiri kwa lugha ya kingereza na kiswahili.


Sehemu ya wazazi waliofika katika mahafalihayo.



Wanafunzi wa shule ya Sirajul Munir wakitoa onesho la skauti katika mahafali hayo.

Afisa rasilimali watu wa The Islamic Foundation, Musa  Buluki akikabidhi cheti kwa mwanafunzi muhitimu wa elimu ya msingi.


Afisa rasilimaliwatu The Islamic Foundatio(TIF) Musa  Buluki kulia  akizungumza jambo na Amiri wa Taasisi ya  SirajulMunir Islamic Center. (SIMC) Abdallaah Kindamba.



Mwalimu Masudi Kaihula akisoma risala mbele ya mgeni rasmi, pembeni aliyemshikia  kipaza  sauti ni  Mwalimu Omari Kisina.





Hili  ni jengo mojawapo la madarasa katika shule ya msingi ya SirajulMunir ambalo limejengwa kwa ufadhili wa  The  Islamic Foundation.




Wazazi waliofika katika mahafali hayo  wakifuatilia michezo mbalimbali kutoka kwa watoto wao.


1 comment:

  1. Kwa shule za Msingi Sirajulmunir wasiliana na Mkuu wa idara ya Elimu Mwalimu Mchau namba ya simu ni 0719569037

    ReplyDelete