Saturday, October 22, 2016

ZAHANATI YA MAKURUNGE WILAYANI BAGAMOYO UAFUNGWA SIKU 4,DAKTARI AENDA KWENYE SEMINA, NESI AENDA LIKIZO, WANANCHI WAKOSA HUDUMA.



Zahanati ya kata ya Makurunge wilayani Bagamoyo ikiwa imefungwa kwa siku 4 mfululizo bila ya kutoa huduma.
.................................


Zahanati ya kata ya Makurunge wilayani  Bagamoyo imefungwa  kwa muda  wa  siku 4 mfululizo bila ya kutoa huduma kutoka na Daktari wake kwenda  kwenye  semina na Nesi kuchukua likizo.

Hali hiyo imebainika baada ya ziara ya mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majidi Mwanga ambae alitembelea katika kata hiyo kwa kushtukiza ili kukagua mambo  mbalimbali.

Mkuu huyo wa wilaya alipofika kitongoji cha gezaulole alipata taarifa kutoka kwa Diwani wa kata ya Makurunge ywa kwamba Zahanati hiyo haijafunguliwa kwa muda wa siku 4 mfululizo jamba ambalo limeleta  kero kwawananchi wa eneo hilo kwa kukosa huduma ya Afya.

Kufuatia hali hiyo,  mkuu wa  wilaya amelazimika kumpigia simu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo Fatma Omari latu, ambapo aliweza kufika katika Zahanati hiyo pamoja na Daktari aliyekuwa kwenye semina.

Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majidi Mwanga amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo kulishughulikia tatizo hilo ili huduma  zipatikane  kama kawaida,  huku  akimtaka mkurugenzi huyo kumchukulia hatua za kisheria Dakatri wa Zahanati hiyo, Paulo Mazinge ili kukomesha tabia hiyo.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya  Makurunge Paulo kabile, alisema hatua hiyo imemsikitisha na  kwamba atahakikisha  Daktari huyo anachukuliwa hatua kwa kiuka  kanuni za kazi na kusababisha usum bufu  kwa wananchi.

Nae mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo, Fatma Omari latu alisema hali hiyo imetokana na kutofuata taratibu  za kazi na kwamba amewaagiza watumishi wote  waliopo ngazi ya kata kutambua  kuwa wanapaswa kutoa taarifa zao kwa mtendaji  kata ili kuepuka kufanya  mambo yatakayokwenda  kinyume na taratibu  za kazi.   



Diwani wa kata ya Makurunge Paulo Kabile akionyesha Kitanda cha kujifungulia mama mjamzito ambacho kinathamani ya zaidi milioni 20 kikiachwa katika usalama mdogo baada milango hiyo kutofunga kwasababu ni mibovu.

Diwani wa kata ya Makurunge Paulo Kabile akionyesha vifaa vilovyotelekezwa katika zahanati ya makurunge baada ya Daktari kwenda  kwenye semina, Nesi kwenda likizo huku milango ikiwa haifungi kutokana na kuharbika vitasa.

Mkuu wa wilaya ya  Bagamoyo, Majidi Mwanga akimpigia simu mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo ili kufika katika Zahanati hiyo kujionea hali halisi.


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo, Fatma Omar Latu akizungumza jambomara baada ya kuwasili katika zahanati ya Makurunge.

Daktari wa zahanati ya makurunge Paulo Mazinge, kulia, akielezea namna alivyoiacha Zahanati hiyo bila ya kutoa huduma mbelei ya mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaji Majidi Mwanga.

Daktari  wa zahanati ya makurunge Paulo Mazinge akiomba msamaha kwa mkuu wa wilaya ya Bagamoyo  Majidi mwanga mara baada ya kutiwa hatiani na kuandaliwa adhabu yake.

No comments:

Post a Comment