Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Mh. Majid Mwanga
akiangalia namna taarifa za wana kaya zinavyoingizwa kwenye mtandao kupitia
simu, wanaoshuhudia wengine kutoka kushoto ni Diwani wa kata ya Makurunge,
Paulo Kabile, na wa pili kushoto ni Mtendaji kata ya Makurunge, Yoel Chumi.
............................................
Zoezi la kuboresha taarifa za wana kaya hapa
nchini zimeanza katika wilaya ya Bagamoyo ambapo mpaka sasa tayari kata tatu
zimerosha taarifa zake, ub oreshaji wa taarifa za makazi wilaya ya Bagamoyo
umeanza kata ya Mapinga, Fukayosi na Makurunge na kuendelea na katza
zilizobaki.
Taarifa za wanakaya zinaboreshwa kutoka kuhifadhi
taarifa kwenye vitabu vya usajili wa makazi vilivyopo kwa wenyeviti wa
vitongoji na sasa taarifa hizo zinaingizwa kwenye mtandao ambapo mwenyekiti
ataweza kuwasiliana na watu wake kupitia simu ya mkononi muda wote.
Uboreshaji huu wa Taarifa utasaidia hata pale mwenyekiti anapohitaji kufanya mkutano na
wananchi wake ujumbe atakaoandika na kuutuma utawafikia wananchi wake wote kwa
wakati mmoja.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Mh. Majidi Mwanga
akipata maelezo ya namna taarifa za wanakaya zitakavyokuwa kutoka kwa mtaalamu
wa takwimu kutoka chuo cha takwimu Dar es Salaam.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majidi Mwanga
akimueleza jambo Diwani wa kata ya Makurunge, Paulo Kabile
Safari ya kutembelea kaya katika kitongojicha
Gezaulole kata ya Makurunge, Kkushoto ni Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Mh. Majid
Mwanga, akiwana mwenyekiti wa kitongoji cha Gezaulole, Tabu luaga na kulia ni
Diwani wa kata ya Makurunge, Mh. Paulo Kabile.
Safari ya kutembelea kaya katika kitongojicha
Gezaulole kata ya Makurunge, Kkushoto ni Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Mh. Majid
Mwanga, akiwana mwenyekiti wa kitongoji cha Gezaulole, Tabu luaga na kulia ni
Diwani wa kata ya Makurunge, Mh. Paulo Kabile.
No comments:
Post a Comment