Tuesday, October 11, 2016

MKAZI WA KIBAHA AENDA JELA MIAKA 30 KWA KUBAKA MTOTO WA MIAKA 4.

Mahakama ya hakimu mkazi Kibaha imemuhukumu mkazi wa maili moja Kibaha, Kulwa Kisitu mwenye umri wa miaka 35 kwenda jela miaka 30 baada ya kutiwa hatianai kwa kosa la kubaka mtoto wa miaka 4 (jina linahifadhiwa).

Mtuhumiwa huyo ambae alikuwa akijihusisha na kubeba  mizigo katika soko la maili moja ametiwa hatiani baada ya mahakama hiyo kujiridhisha na ushahidi uliowasilishwa na upande wa Jamhuri.

Mwendesha mashtaka wa serikali, Rashidi Chamwi aliiambia mahakama hiyo kuwa, mtuhumiwa Kulwa Kisitu ambae anaishi nyumba moja na bibi na babu wa mtoto huyo alimbaka mtoto huyo alimbaka mtoto huyo mnamo Tarehe 28-05-2016 majira ya jioni, wakati alipokuwa ameachwa na bibi yake.

Mwendesha mashtaka huyo ameongeza kuwa, mtuhumiwa alianza kuchezesha uume wake kwenye sehemu za siri za mtoto huyo na  alipoona hamalizi haja yake ndipo alipoamua kujaribu kumuingiza mtoto huyo ndani na alipoona mtoto huyo anapiga kelele aliamua kuacha.

Mtoto huyo alibainika  kuingiliwa wakati bibi yake aliporejea na kuanza kumuogesha ndipo mtoto huyo akamtaja Kulwa Kuwa ndiye aliyefanya tukio hilo.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu mkazi wa Mahakama ya  Kibaha, Aziza Mbadyo amesema mahakama hiyo imeridhika na ushahidi uliotolewa mahakani hapo na kutoa adhabu ya miaka 30 jela ili kuwa fundisho kwa wengine.

Awali mtuhumiwa huyo aliomba mahakama hiyo kumpunguzia adhabu kwani hata yeyeanajutia kosa alilofanya kwakuwa ni tamaa tu za mwili na shetani alimpitia.   

No comments:

Post a Comment