Kushoto ni
Mkurugenzi wa shule ya msingi MWASAMA iliyopo Bagamoyo, Mwajuma Saidi
Masaiganah akiwa na wageni wake mara walipotembelea katika shule ya MWASAMA,
kulia ni Agnes Weber na katikati ni Bernd Sdiapers.
Mkurugenzi wa shule ya msingi MWASAMA, Mwajuma Saidi Masaiganah akiwa na
wageni wakeofisini kwake mara walipowasili shuleni hapo kujionea maendeleo ya
shule hiyo.
..........................................
Wadau wa elimu kutoka chuo kikuu cha sayansi cha
Ujerumani, wametembelea shule ya msingi ya
MWASAMA iliyopo Bagamoyo ili kuona mafanikio yanayopatikana katika shule
hiyo.
Akizungumza mara baada ya kuwapokea wageni
hao, mkurugenzi wa shule ya MWASAMA, Mwajuma
Saidi Masaiganah alisema anawasukuru wadau hao wa elimu kwa kufika katika shule hiyo ili
kubadilishana uzoefu na michango mbalimbali katika maendeleo ya elimu.
Aidha, alitumia nafasi hiyo kutoa shukrani zake
kwa wadau hao ambao waliweza kufadhili ujenzi wa madarasa mawili, Vitabu vya
sayansi, pamoja na umeme wa sola ikiwa kama mchango wao kwa shule hiyo.
Mkurugenzi huyo washule ya MWASAMA alisema kuwa
wadau hao wa elimu licha ya kutoa msaada
huo katika shule hiyo pia wameweza kutoa msaada wa vitabu katika shule
mbalimbali hapa nchini wakiwa na lengo kuonyesha namna wanavyothamini sekta ya
elimu.
Mwajuma aliwaeleza wageni hao kuwa licha ya changamoto mbalimbali zinazoikabili shule hiyo, wamefanikiwa kushika nafasi ya 1 wilaya kati ya shule 13 zilizopo kwenye kundi hilo, nafasi ya 1 mkoa kati ya shule 323 katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba 2016 huku kitaifa ikishika nafasi ya 33 kati ya shule 8241.
Alisema mafanikio hayo yamepatikana kutokana na ushirikiano na wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo wao ambao wameweza kusadia kutatua baadhi ya changamoto shuleni hapo.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake, mhadhiri wa
chuo kikuu cha Sayansi kutoka ujerumani,Bernd Sdiapers alisema ujio wao
katikashule hiyo umetokana na namna uendeshaji wa shule hiyo unavyozingatia
thamani ya kumpa mtoto elimu.
Alisema ili jamii iweze kutekeleza mambo
mbalimbali ya kimaendeleo inahitaji kuwa na
elimu, hivyo kitendo cha kuwapa watoto elimu kinahitaji kuungwa mkono na wadau mbalimbali
wa elimu ili kuwa na jamii yenye wataalamu wa fani mbalimbali.
Aidha, aliipongeza shule ya MWASAMA kwa kushika
nafasi ya kwanza wilaya ya Bagamoyo, katika matokeo ya mtihani wa darasa la
saba mwaka 2016.
Alisema hiyo ni kazi nzuri in ayofanywa na
mkurugenzi Mwajuma Saidi Masaigana na kwamba alimtaka asikate tamaa katika
kutekeleza majukumu yake.
Katika ziara yao wadau hao waliweza kuona maonyesho mbalimbali kutoka kwa
wanafunzi wa shule hiyo na kufurahishwa namna watoto hao walivyoweza kuonyesha umahiri wao katika mambo
mbalimbali.
Wadau wa elimu kutoka Ujerumani wakimsikilza
mwenyeji wao, Mkurugenzi wa shule ya msingi
MWASAMA, Mwajuma Saidi
Masaiganah, hayupo pichani, kutoka kulia ni Bernd Sdiapers, wa pili kulia ni
Agnes Weper na wa kwanza kushoto ni Sebasitian Schramm.
Walitembelea eneo lote lashule ili kujionea mambo
mbalimbali katika shule hiyo, kulia ni Mkurugenzi wa shule ya MWASAMA, Mwajuma
Saidi Masaiganah, katikati ni Bernd Sdiapers, na wa kwanza kushoto ni Sebastian
Schramm.
Wageni hao
walitembelea ujenzi wa bweni lawanafunzi, kushoto ni Makamo mwenyekiti wakamati
ya shule hiyo, Hamza Mfaume anaefuata ni mwalimu mkuu wa shule hiyo Hamza
Mapesa wakiwa na wageni wao.
Kushoto ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Hamza
Mapesa wa pili kushoto ni Makamo mwenyekiti wa kamati ya shule, Hamza Mfaume na
mgeni wao Bernd Sdiapers
Kutoka kushoto ni Bernd Sdiapers, katika ni
Sebastian Schramm na wa kwanza kulia ni
Agnes Weber wakiangalia michezo kutoka
wanafunzi wa shule hiyo.
Mkurugenzi wa shule ya msingi MWASAMA, akiwa na
wageni wake wakiangalia wanafunzi wakinyesha michezo ya utamaduni.
Kikundi cha ngoma kutoka Taasisi ya Sanaa na
Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) wakitoa burudani kwa wageni
Wanafunzi wa shule ya msingi MWASAMA wakitonyesha
umahiri wao katika mambo utamaduni na sanaa mbele ya wageni
Wanafunzi wa KG nao wakifuatilia kinachoendelea.
Wanafunzi wa shule ya msingi MWASAMA wakiimba
wimbo wa Tanzania Tanzania
Picha ya pamoja kabla ya kuondoka.
Kutembelewa na maadili Hawa kumetupa faraja. Nd. Bernd Shoppers alikuwa Mwalimu wa sayansi kwenye iliyokuwa shule rafiki ya Real Schulle Shuleni ya Ujerumani. Aliwezesha wanafunzi wake kuchangisha fedha na kununua vifaa Vya sayansi Vya kufundishia wanafunzi wetu na kulea mtambo wa solar kwa gharama zao na mafundi wao.
ReplyDeleteShule ya Mwasamainavyo vifaa Vya kutosha na inakaribia Vyuo na vyuo vikuu Vya Bagamoyo vinavyotoa waalimu wa sayansi waje kufanyiwa mafundi kazini kwetu ili vifaa hivi viti Mike kwa taifa ya taifa hili. Mashirikiano katika sekta ya elimu ni muhimu katika kutoa elimu Bora na si Bora elimu. KARIBUNI sana tuijenge Tanzania yenye wanasayansi bora duniani.