Saturday, October 22, 2016

MUUGUZI HOSPITAL YA WILAYA YA CHUNYA MBEYA ATIWA MATATANI KWA TUHUMA ZA KUSABISHA KIFO CHA MTOTO MCHANGA

Patricia Kisoti Muuguzi anayetuhumiwa kufanya uzembe uliosababisha Mama mjamzito kujifungua na mtoto wake kupoteza maisha katika hospital ya Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya.
 

Mkuu wa Wilaya ya Chunya Rehema Madusa akizungumza na watumishi wa hospital ya Wilaya ya Chunya kufuatia tukio la mama mjamzito kifanyiwa vitendo vya unyanyasaji na mmoja wa watoa huduma hospitalini hapo hali iliyopelekea mtoto kupoteza maisha.
 

Mkuu wa Wilaya ya Chunya Rehema Madusa akimfariji Maria Solomoni ambaye alipoteza mtoto wake   kwa uzembe wa muuguzi katika katika hospital ya Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya.
 

Mkuu wa Wilaya Chunya Rehema Madusa akiwa na majonzi baada ya kumsikia mama aliyepoteza mtoto wake mara baada ya kujifungua kutokana na uzembe wa muuguzi katika hospital ya Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya. 
 

Baadhi ya watumishi wa hospital ya Wilaya ya Chunya katika Mkutano na Mkuu wa Wilya ya chunya mara baada ya kutokea tukio la mama mjamzito aliyepoteza mtoto wakati akijifungua kutokana na uzembe wa mmoja wa wauguzi hospitalini hapo.
 

Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo ya Wilaya ya Chunya,
Sasita Shabani akizungumza kuhusiana na tukio hilo la kufanyiwa ukatili kwa mama mjamzito na mmoja wa wauguzi.
 

Wananchi na wanaopata huduma za afya katika Hospita ya Wilaya Chunya wakionesha nyuso za majonzi mara baada ya mmoja wa wananchi kufanyiwa vitendo vya kikatili.
 

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chunya,
Sophia Kumbuli akisisitiza jambo kuhusiana na tukio hilo.

No comments:

Post a Comment