Diwani wa kata ya Bunju, Kheri Nasoro alipokuwa katika harambee ya kuchangia ujenzi wa msikiri.
....................................................
Harambee ya kuchangia ujenzi wa msikiti katika mtaa wa Boko beach imefanikisha kukusanya milioni tatu na laki mbili, 3,200,000/= ikiwa ni pesa taslimu pamoja na ahadi huku Diwani wa kata ya Bunju Kheri Nasoro, akiwa amechangia kiasi cha shlilingi milioni moja katika ujenzi huo wa Msikiti.
Akizungumza katika Harambee hiyo iliyofanyika
katika eneo linalotarajiwa kujengwa msikiti mtaa wa Boko beach Diwani wa kata
Bunju Kheri Nasoro amesema atashirikiana na uongozi wa Swafatul mukarama ambao
ndio wasimamizi wa ujenzi huo ili kuhakikisha ujenzi huo unakamilika.
Alisema wailsamu wanapaswa kutambua kuwa jambo
hilo ni lao na kwamba kila mmoja
ajitolee kulingana na uwezo wake ili kufikia malengo.
Katika harambee hiyo mada za umuhimu wakutoa
ziliwasilishwa ambapo Ustadhi, Hashim Rajabu kutoka Masjid Fatmat Zaharaa Boko,
alisema waislamu wanapaswa kutambua kuwa kutoa katika njia ya kheri ni
kujiwekea akiba ambayo itamsaidia mwenyewe siku ya malipo.
Akinukuu Hadithi ya Mtume
Muhammad Swalallaahu Alayhi Wasallama, Ustadhi, Hasim alisema ''Mwenye
kujnga msikiti, Mwenyezimungu atamjengea nyumba peponi'' hivyo aliwataka
waislamu kukimbilia kheri hiyo kwaajili ya kutengeneza Akhera yao.
Nae Ustadhi Omari Jumakutoka masjid Rrahmani
Tegeta, alisema swala la kutoa katika njia ya Mwenyezimungu linahita imani na
wala si kipato kikubwa kama ambavyo wengi wanadhani.
Ustadhi Omari alitolea mfano wa baadhi ya matajiri wanaodhamini mashindano warembo na michezo
ya mpira kwa gharama kubwa huku wakiwa hawana habari na dini ya Allaah katika kuipigania.
Aliongeza kwa kusema kuwa swala la kutoa katika njia ya mwenyezimungu ni jihadi ndiyo mana katika aya kadhaa
ndani ya Qurani Mwenyezimungu amesema kupigana jihadi kwa mali zenu na
nafsi zenu, hii inonesha uzito wa kutoa
hali iliyopelekea kuwekwa katika darja
ya jihadi.
Aliendelea
kwa kusema kuwakila neema itaulizwa,
hivyo muislamu asidhani kwakumiliki kwake fedha anayo fursa ya kutumia
anavyotaka, bali anapaswa kutumia fedha
kwa mujibu Allaah anavyotaka kwakuwa
kwake yeye zimepita kama wakala
hivyo ataulizwa namna alivyozitumia.
Akifunga
Harambee hiyo, katibu wa Swafatul
Mukarama Abduli Said Shomari alisema katika siku ya kwanza ya harambee hiyo wameweza
kukusanya kiasicha shilingi mioni 3 na
laki mbili ikiwa fedha taslimu pamoja na
ahadi.
Katibu huyo ametoa wito kwa waislamu
kuendelea kuchangia ujenzi huo wa msikiti ambao utagharimu shilingi milioni mia tano na arubaini na saba, laki
moja themanini na nne mia sita na tano, hadi kukamilika kwake, 547,184,615/=
Aidha, alitaja namba kwa
watakaokuwa tayari kuchangia wanaweza kuchangia kupitia tigo pesa 0673 976336,
Airtel money 0682982111, au akaunti benki, 003140405030001 Benki ya Amana, akauti zote hizo zinajulikana kwa
jina la Masjid Swafatul-Mukarama.
Kwa maelezo zaidi wasiliana kwa namba 0784070891 katibu wa Bodi amba 0713422774 Mwenyekiti namba 0713326287.
Kwa maelezo zaidi wasiliana kwa namba 0784070891 katibu wa Bodi amba 0713422774 Mwenyekiti namba 0713326287.
No comments:
Post a Comment