Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, kushoto Majidi Mwanga
akikagua shule ya sekondari Kiwangwa, kulia ni makamo mkuu wa shule ya
Sekondari Kiwangwa, Robadi Uzageni.
.............................
.............................
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majidi Mwanga atembela
ghafla shule ya Sekondari Kiwangwa ili kuangalia utendaji kazi na changamoto
mbalimbali zinazoikabili shule hiyo.
Katika ziara hiyo mkuu huyo wa wilaya aligundua
mambo kadhaa, ikiwemo utoro wa walimu, upungufu wa matundu ya choo na tatizo la
maji ambpo wanafunzi huchota maji umbali mrefu.
Mkuu huyo wa wilaya alisema kitendo cha kufuata maji umbali mrefu kwa wanafunzi kuna matatizo kadhaa yanayowakuta ikiwa
ni pamoja na kuchelewa vipindi darasani,
hatari ya kuviziwa na wavulana nje ya shule hali itakayopelekea wasichana
kupata mimba na maumivu ya kubeba ndoo.
Wakizungumzia adha wanayoipata katika kuchota maji wanafunzi hao wamesema
kuwa wanatumia umbali mrefu kufuata maji na kwama wakifika kisimani kunakuwa na
foleni kubwa kwakuwa kisima hicho hutumiana wananchi wengine hali inayopelekea
kuchelewa masomo.
Wameongeza kuwa endepo mwanafunzi akifanya kosa na akapewa adhabu ya kuchota maji atakaa
siku nzima anachota maji kulingana umbali wa kufuata maji.
Aidha, wasichana katika shule hiyo pia wamekiri
kuwepo kwa tabia za wanaume wa mitaani kutumia nafasi hiyo kuwasumbua njiani
hali inayopelekea kuhofia usalama wao wa kiafya na kuharibikiwa kimasomo kwani
wanaweza kuingia kwenye mapenzi bila ya kutarajia kutokana na mazingira.
Kwa upande wake makamo mkuu wa shule ya Sekondari
Kiwangwa Robadi Uzageni, alikiri kuwepo kwa tatizola maji katika shule hiyo
hali inayopelekea wakati mwingine kukatisha vipindi ili wanafunzi wakapate
maji.
Alisema kutokana na halihiyo wakati wanafunzi
hutolewa jioni kwnda kuchota maji na
huchukua muda mrefu kwenye foleni kutokana na umbali lakinipia visima
hivyo hutumka pia na wananchi wa vijiji vya Bago na Kiwangwa hali inayopelekea
wanafunzi kukosa chakula kwakuwa hutumia
muda mrefu kwenye maji mpaka muda wakula
unawapita wakiwa huko.
Mwalimu Uzageni alitumia nafasi hiyo kuwaomba wadau mbalimbali wa maendeleo kuisadia shule
sekondari kiwangwa ili ipate maji iweze kuondokana na adha ya kutafuta maji
umbali mrefu jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa wanafunzi.
Kufuatia hali hiyo mkuu wa wilaya ya Bagamoyo,
Majidi Mwanga amewaomba wadau mbalimbali
kuchangia upatikanaji wa maji katika shule hiyo ili kuwaondolea adha wanafunzi wanosoma katika shule hiyo.
Aidha, mkuu huyo wa wilaya ameishukuru Taasisi ya
The Islamic Foundation (TIF) yenye makao yake
makuu mkoani Morogoro, kwa kusaidia visima katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Bagamoyo na
kumuomba mwenyekiti wa The Islamic Foundation, Aref Nahdi kuangalia uwezekano wa
kuwapatia maji shule ya sekondari Kiwangwa.
Taasisi ya The Islamic Foundation ya mjini Morogoro ni miongoni mwa taasisi
zilizochangia upatikanaji wamaji katika wilaya ya Bagamoyo ambapo kuanzia mwaka
2006 imeweza kuchimba visima 220 kati ya hivyo vipo virefu na vifupi ambavyo
vimegharimu zaidi ya milioni 800.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga
akisalimiana na wanafunzi wa shule ya Sekondari Kiwangwa huku akiwasisitiza
kusoma kwa bidii.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga
akielekea katika kisima ambacho
wanafunzi wa shuleya sekondari wanapata maji, kushoto ni makamo
mkuu wa shule ya Sekondari Kiwangwa, Robadi Uzageni.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majidi Mwanga akiingia
kwenye eneo la kisima ambacho wanafunzi wanachota maji.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, majidi mwanga
akichota maji kwenye kisima kwa kutumia kata ya kuchotea.
Mkuu wa wilaya ya
Bagamoyo Majidi Mwanga akikokota Baiskeli kutoka kisimani hali ambayo
wananchi wa kijiji cha Bago hutumia baiskeli kubebea maji.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Kiwangwa
wakitoka kuchota maji umbali mrefu kutokana na shule hiyo
kukosa maji.
No comments:
Post a Comment