Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli, kesho tarehe 31 Oktoba, 2016 ataanza ziara ya Kiserikali
ya siku mbili nchini Kenya kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta.
Rais Magufuli anatarajiwa
kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Jijini Nairobi majira ya saa nne asubuhi na baadaye kupokelewa rasmi na
mwenyeji wake Rais Kenyatta katika Ikulu ya Nairobi ambako viongozi hao
watafanya mazungumzo rasmi.
Pamoja na kufanya
mazungumzo rasmi na mwenyeji wake, Rais Magufuli atakwenda kutoa heshima katika
Kaburi la Rais wa Kwanza wa Kenya Hayati Mzee Jomo Kenyatta na pia anatarajiwa
kuhudhuria dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta
Ikulu Jijini Nairobi.
Ikulu Jijini Nairobi.
Katika ziara hii Rais
Magufuli anatarajiwa kutembelea kiwanda cha maziwa cha Eldoville
kilichopo Karen Jijini Nairobi, na pia anatarajiwa kuzindua barabara mchepuko
ya Southern By-pass iliyopo Jijini Nairobi.
Barabara hiyo mchepuko ya Southern By-pass ni moja kati ya miradi mikubwa ya barabara nchini Kenya, inaunganisha maeneo mbalimbali ya Jiji la Nairobi kwa barabara za juu na chini na imejengwa kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari katika Jiji hilo.
Rais Magufuli anatarajiwa
kumaliza ziara yake tarehe 01 Novemba, 2016 na kurejea Jijini Dar es Salaam.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano
ya Rais, IKULU
Nairobi 30 Oktoba,
2016.
2016.
No comments:
Post a Comment