Tarehe 21 Oktoba, 2016 saa 3:00 asubuhi Naibu Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe. Balozi Hassan Simba Yahya
anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za mahafali ya 13 ya Kidato cha Nne
katika Shule ya Sekondari ya Bwawani iliyopo Mkoa wa Pwani.
Shule ya Sekondari Bwawani inamilikiwa na Jeshi la
Magereza, ilianzishwa mwaka 1978 kwa lengo la kutoa elimu ya Sekondari kwa
Watumishi wa Magereza ambapo hivi sasa Shule hiyo inatoa elimu ya Sekondari kwa
vijana wa kike na kiume kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini.
Shule hiyo pia inatoa elimu ya Kidato cha Tano na
Sita, katika muunganiko wa masomo ya Historia, Jiografia na Kiswahili (HGK),
Historia, Jiographia na Kiingereza(HGL).
Aidha, mwaka huu inatarajia kuanzisha
mkondo wa masomo ya sayansi(CBG) yaani masomo ya Kemia, Baiologia na Jiografia.
Jumla ya Wanafunzi 94 wa shule hiyo wanatarajia
kuhitimu elimu yao ya kidato cha nne mwezi Novemba mwaka huu.
Sherehe hizo zitajumuisha mambo yafuatayo:-
- Mgeni rasmi kutembelea maeneo ya shule na kuweka mawe ya ufunguzi katika majengo ya shule;
- Mgeni rasmi kuangalia Maonesho ya Taaluma kwa Wanafunzi Washiriki;
- Mgeni rasmi kutoa vyeti na zawadi mbalimbali kwa Wanafunzi wahitimu na;
- Mgeni rasmi kutoa hotuba
Sherehe za mahafali hayo zinatarajia kukamilika saa
8:00 mchana. Vyombo vya Habari vinakaribishwa kwenye sherehe hizo tarehe 21
Oktoba, 2016 kuanzia saa 3:00 asubuhi.
Imetolewa na: Lucas Mboje,
Mrakibu Msaidizi wa Magereza,
Afisa Habari wa Jeshi la Magereza,
DAR ES SALAAM
20 Oktoba, 2016.
No comments:
Post a Comment