Wahitimu waelimu ya Msingi katikashule ya msngi
ya yemen iliyopo Chang'ombe jijini Dar
es Salaam.
Muasisi wa Shule za DYCCC Salim Baabae
akizungumza katika mahafali hayo
....................................................
Wazazi na walezi wametakiwa kudumisha malezi bora wanayopata watoto wao katika shule za
kiislamu ili kuweza kupata Taifa lenye viongozi wenye maadili katika jamii.
Wito huo ume umetolewa na muasisi wa shule za
yemeni, Salim Baabae, alipokuwa akizungumza katika mahafali ya wahitimu wa darasa la saba washule ya msingi Yemeni
English Medium yaliyofanyika katika viwanja vya shule hiyo iliyopo eneo la Chang'ombe
jijini Dar es Salaam.
Salim
Baabae ambae ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo amewataka wazazi na walezi
kuhakikisha wanadumisha malezi na tabia njema walizopata watoto wao walipokuwa
shule ya msingi ili malezi na tabia hizo
ziendelee katika maisha yao yote.
Aidha, amewataka wazazi na walezi kuwa makini na
vitu vya kuwanunulia watoto wao ili kuepuka kuwanunulia vifaa vitakavyowatoa
kwenye maadili na kupoteza malengo yao yabadae.
Alisema katika kipindi hikicha utandawazi, watoto
wengiwamekuwa wanamiliki, simu, I pad, na mfano wa hivyo ambavyo kwa kiasi
kikubwa vinachangia katika mmomonyoko wa maadili katika jamii huku vitu hivyo
vikichangia katika kufeli kwa watoto kwakuwa muda mwingi wanashughulishwa na matumizi ya simu
na I pad kuliko kufuatilia masomo.
Aliongeza kwa kuwataka wazazi na walezi kuchagua
shule zenye kutoa elimu bora kwaajili ya masom o ya sekondari ili wasipoteze
taaluma waliyopata watoto wao ambapo aliwataka wazazi na walezi kuwaacha watoto
katika shule ya sekondari ya Yemeni ili waendeleze taaluma namalezi bora
waliyopata shuleni hapo.
Nae mwenyekiti wa Bodi ya Shule, Hassan Akrabi,
amesema mafanikio yaliyopatikana katika shule za Yemeni ni kutokana kuwa na
mahusiano mazuri na jamii yote
kwa ujumla huku akitoa shukrani zake kwa
vyombo vya Habari vya Imaan Media pamoja na uongozi wa The Islamic Foundation
ukiongozwa na Mwenyekiti wake Aref Nahdi kwa kushirikiana katika fikra
za kupiga hatua kimaendeleo.
Alisema Imaan Media pamoja na TIF kwa ujumla imekuwa na mchango mkubwa
hasa pale inapohitajika kutoa fikra za kimaendeleo ambapo mwenyekiti wake Arif
Nahdi amekuwa mwepesi kuonesha ushirikiamno.
Mwenyekiti huyo wa Bodi ya shule aliwataka wazazi
na walezi wa shule hiyo kuunga mkono juhudi zinazofanywa na uongozi wa shule
ili kufikia malengo ya kuwalea watoto
kielimu na kimaadili.
Alisema katika kuunga mkono juhudi ni pamoja na
kulipa ada kwa wakati ili kuepuka watoto kurudishwa nyumbani kwaajili ya ada
jambo ambalo linarudisha nyuma taaluma ya mtoto.
Awali akizungumza mbele ya mgeni rasmi mwalimu
mkuu wa shule ya msingi Yemen English Medium, Rahimu Burhani, amesema shule
hiyo imejipanga kuboresha Taaluma ambapo
mwalimu mmoja anafundisha watoto wasiozidi 30, ili kila mtoto aweze
kuelewa vizuri anachofundishwa darasani.
Alisema shule
hiyo imejiandaa kuongeza wanafunzi zaidi kwakuwa tayari wanavyo vyumba vya madarasa ambavyo havina wanafunzi na kuwataka wazazi, walezi na jamii kwa ujumla
kuwaunga mkono kwa kupeleka watoto wao
ili wapate elimu yenye manufaa.
Jumla ya wanafunzi 110 wamehitimu elimuya msingi
katika shule ya msingi ya Yemen ambao kati
yao wavulana ni 48 na wasichana ni 62.
Jumuiya ya D.Y.C.C.C. inamiliki shule shule yaawali, shule ya
msingi, pamoja na shule ya sekondari,
Baadhi ya wazazi wakiwa katikamahafalihayo
Mwen yekiti wa Bodi ya shule za Yemen, Hassan Akrabi
katikati, kushoto ni muasisi wa shule hizo Salim Baabae, na kulia ni
mjumbe bodi Salmin Aljabry.
Wanafunzi wa darasa la
kwanza katika shule hiyo
Kulia ni mwenyekiti wa Bodi ya Shule za DYCCC
Hassan Akrabi katikati ni muasisi washule za DYCCC Salim Baabae na kushoto ni
mwalimu mkuu wa shule ya Yemen English
Medium, Rahimu Burhani.
Mgeni
rasmi, ambae ni muasisi wa shule za DYCCC Salim Baabae akimkabidhi
zawadi mwanafunzi, kulia ni mwenyekiti wa bodi ya shule Hasan Akrabi, na wa
kwanza kushoto ni mkuu wa shule hiyo Rahimu Burhani
Sehemu ya majengo ya shule za DYCCC eneo la
Chang'ombe jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment