Bibi Abella Bateyunga (kulia) kutoka Tanzania Bora
Initiative akipokea hundi ya shilingi milioni mia mbili na tisa elfu hamsini na saba mia sita sabini na nne, 209,057,674. ikiwa ni ruzuku ya Vijana kwaajili ya kujiendeleza, kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila, wa pili ni Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akifuatiwa na Mkurugenzi wa Mission wa USAID, Andrew Karas, kutoka sekta binafsi ni Mtaalamu wa Mradi wa Vijana, Joyce Mndambi, (PICHA NA UBALOZI WA MAREKANI).
Mkurugenzi wa Mission wa USAID, Andrew Karas, akizungumza katika hafla hiyo ya kukabidhi hundi kwa vijana iliyofanyika Mkoani Mbeya. (PICHA NA UBALOZI WA MAREKANI).
....................................
Serikali ya Marekani imetoa misaada yenye thamani ya dola
750,000 kwa taasisi tisa ambazo zinasaidia utengenezaji wa ajira, ujasiriamali,
uongozi, na maisha bora kwa vijana.
Misaada hiyo imetolewa na mradi wa Inua Vijana wa Feed the
Future Tanzania , inayofadhiliwa na Serikali ya Marekani kupitia Shirika la
Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID), na wanatarajia kutengeneza ajira
950 kwa vijana katika makampuni 700 mapya au ambayo yanaongozwa na vijana
katika mikoa ya Iringa, Mbeya, na Zanzibar.
Mkurugenzi Mkazi wa USAID, Andrew Karas, na Mheshimiwa
Suleiman Jafo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (TAMISEMI), walikabidhi misaada hiyo kwa taasisi husika.
Wakati wa hotuba yake, Bwana Karas alibainisha kuwa “Kuwekeza
katika uongozi wa vijana nchini Tanzania ni kipaumbele cha USAID na Serikali ya
Tanzania.
"Asilimia kubwa ya Watanzania ni vijana, na idadi ya
wananchi wake inatarajiwa kuongezeka mara mbili ndani ya miaka 25 hadi 30
ijayo.
Jitihada za makusudi zinahitajika kwa serikali, sekta
binafsi na jamii ili kuhakikisha kuwa nguvu, vipaji, na matumaini ya vijana wa
leo, pamoja na kizazi kijacho, zinafanya Tanzania kuwa mahali pa mafanikio kwa
wote.”
Mradi wa Inua Vijana unahamasisha vijana wa vijijini
kushiriki katika sekta ya kilimo nchini Tanzania na kuwapatia fursa za kiuchumi
vijana wenye umri wa miaka 15-35 pamoja na kuhamasisha uongozi na mienendo ya
kiafya.
Kupitia misaada hii, Inua Vijana ya Feed the Future Tanzania
itabadili changamoto kuwa fursa kwa vijana wa vijijini kuongoza na kushiriki
katika ukuaji wa uchumi wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment