NA
HADIJA HASSAN, LINDI.
Waziri
wa nishati Medadi kalemani amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la umeme
Tanzania TANESCO kwa kushirikiana na meneja wa Tanesco Mkoa wa Lindi
kuhakikisha umeme katika wilaya ya Ruangwa unaendelea kuwa imara na bora wakati
wote.
Waziri
kalemani ameyasema hayo jana mei 20 alipokuwa katika kata ya chinongwe
Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi wakati akzungumza na wakazi wa kata hiyo katika hafla
fupi ya uwashwaji wa umeme kijijini hapo katika shule ya Sekondari chinongwe.
Alisema
katika kutekeleza Miradi ya umeme vijijini REA Serikali tayari imeshatoa kiasi
kikubwa cha fedha hivyo ni wajibu wa watendaji kusimamia miradi hiyo kwa
ufanisi.
“kama
serikali tumetumia hela nyingi ili kuondokana na matumizi ya kununua mashine
pamoja na mafuta kwa ajili ya kuendeshea mitambo ya kuzalishia umeme ili kurekebisha
hali ya upatikanaji wa umeme katika Wilaya ya Ruangwa na maeneo ya jirani”.
Alisema
ni muhimu kwa mameneja wa shirika hilo kuhakikisha umeme unakuwa wa uhakika
katika vijiji vyote vilivyounganishiwa umeme kupitia mpango wa Umeme Vijijini
REA.
Pamoja
na mambo mengine Dkt Kalemani aliwataka wananchi wa wilaya ya Ruangwa na maeneo
mengine kutumia fursa ya umeme wanaounganishiwa katika kuanzisha shughuli za
kiuchumi ikiwa ni pamoja na kuanzisha viwanda vidogo vidogo Wakizungumza kwa
nyakati tofauti wakazi wa kata hiyo akiwemo mwajuma nambambo na Asha saidi
wameishukuru Serikali kwa kuwaletea nishati ya Umeme katika maeneo yao ambao
utawafanya kuanzisha shughuli mbalimbali za kiuchumi kwa kutumia umeme huo.
Awali
akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa REA kwa awamu ya tatu meneja wa
Tanesco Wilaya ya Ruangwa Pyuza Samwel alisema kuwa katika kutekeleza mradi huo
wilaya ya Ruangwa inatarajia kunufaika katika vijiji 34 ambapo mpaka sasa
tayari vijiji 16 vimeshawasha umeme huo, huku akisema kuwa katika mradi huo pia
unatarajiwa kujenga njia kubwa ya umeme 33kv(km) 117.74 na kueleza kuwa kazi
iliyofanyika mpaka sasa ni km 90.9 sawa na asilimia 77.12%.
Alizitaja
kazi zingine zinazotakiwa kufanyika kuwa ni ujenzi wa njia ndogo ya Umeme LV km
106.6 ambapo kazi iliyofanyika ni km 10.15 sawa na 10.18%, Transfoma 50kva 50
ambapo tayari transfoma 18 zimeshawekwa sawa na asilimia 18%
No comments:
Post a Comment