Amana
Bank kwa kushirikiana na Mtandao wa simu za mkononi wa Vodacom kwa pamoja
wamezindua huduma mpya ijulikanayo kama ''halal pesa''.
Huduma
hii mpya sasa itapatikana kwa wateja wa Vodacom wanaotumia M-Pesa na wale wa
Amana Bank kwa kuzingatia misngi ya sheria ya kiislamu.
Akizungumza
katika uzinduzi wa huduma hiyo, Mkurugenzi mtendaji wa Amana Bank, Dkt. Muhsin
Salim Masoud, alisema kwa muda mrefu wamekuwa wakifikiria jinsi ya kuwafikia
wateja wengi zaidi ambao wanapenda kutumia miamala ya kifedha kwa mujibu wa
sheria ya kiislamu.
Dkt.
Muhsin alisema Amana Bank imekuwa ikibuni njia mbalimbali za kuwafikia wateja
wake wazamani na wapya hivyo wameweza kuanzisha huduma hiyo ya halal pesa
ambapo wateja wa Vodacom wanaotumia M-pesa wataipata huduma hiyo mpya
inayozingatia misingi ya sheria ya kiislamu.
Alisema
katika huduma ya halal pesa mteja wa Amana Bank anaweza kufanya miamala yake
kwa kutumia Vodaco M-Pesa huku akiwa bado yupo kwenye sheria za uislamu kuhusu
miamala ya kifedha.
Akifafanua
zaidi Dkt. Muhsin alisema Amana Bank imetimiza miaka minane mpaka sasa na
kwamba katika kipindi chote hicho toka kuanzishwa kwake imekuwa ikiendesha
shughuli zake kwa mujibu wa sheria za kiislamu.
Alisema
Benki hiyo ndio benki pekee hapa Tanzania ambayo mfumo wake wa kifedha
umesimamia sheria za benki za kiislamu.
Hata
hivyo aliongeza kwa kusema kuwa, licha ya Benki hiyo kufuata sheria za kiislamu
katika uendeshaji wake, bado inaendelea kuwahudumia wateja wake bila ya kubagua
dini, rangi wala kabila hivyo amewataka wateja wao kutambua kuwa Benki hiyo ipo
kwaajili ya kila mtu.
Alisema
kuanzishwa kwa huduma ya halal pesa kwa kushirikiana na mtandao wa simu wa
Vodacom kutasaidia watu wengi zaidi kufikiwa na huduma giyo ambayo inafuata
sheria za kiislamu.
Kwa
upande wake Mkuu wa kitengo cha huduma za M-Pesa kutoka Vodacom, Tulisindo
Rashid alisema, halal pesa imelenga zaidi ya robo tatu ya waislamu nchini
Tanzania ambao kwa kupitia mfumo wa M-Pesa wataweza kuweka fedha na kupata
faida kihalali (bila ya riba).
Alisema
kwa muda mrefu waislamu wamekuwa na uhitaji mkubwa wa huduma za kuweka fedha
zinazfuata sheria za dini ya kiislamu ambapo huduma hiyo itawezesha watumiaji
wake kuweka fedha kwa njia rasmi ya halal pesa.
Alisema
Vodacom itaendelea kutoa ufumbuzi wa mambo mbalimbli ili kukidhi mahitaji ya
wateja wake katika mfumo wa kifedha kwa kutumia teknolojia ya kidigitali yenye
gharama nafuu na uwezo wa hali ya juu.
Aliongeza
kwa kusema kuwa, halal pesa ni huduma rahisi na ya kipekee inayoendana na
sheria za kiislamu ambayo imegawanyika katika mafungu mbalimbali.
Alifafanuwa
kuwa, mafungu hayo ni pamoja na kuweka pesa binafsi, kwaajili ya kwenda hija,
watoto au kuweka pesa kwa muda mrefu kuanzia miezi 3 hadi 12.
Aidha,
alitumia nafasi hiyo kutoa wito kwa maimamu wa misikiti kufungua Akaunti
kupitia halal pesa ambapo msikiti utapewa namba maalum ya utambulisho (Code
number) itakayowawezesha waumini kuchangia michango ya msikiti hata kama hawapo
msikitini.
Alisisitiza
kuwa, huduma hiyo ni salama na kwamba inafuata misingi ya kiislamu kwa kupata
muongozo kutoka kwa wanazuoni wa kiislamu kuhusu masuala ya kifedha.
Sheria
ya kiislamu imeharamisha riba na kuhalalisha biashara hivyo muislamu anapofanya
miamala ya kifedha huchunga mipaka ya kisheria na kujiepusha na riba.
Kwa
huduma hii mpya ya halal pesa iliyozinduliwa kwa ushirikiano wa Amana Bank na
Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom itamuwezesha muislamu kuweka fedha Amana
Bank na kuzitoa kwenye M-Pesa huku akiwa hakutani na riba na badala yake
atapata gawio la faida ambalo limeruhusiwa katika sheria ya uislamu.
Mkurugenzi mtendaji wa Amana Bank, Dkt. Muhsin
Salim Masoud, akizungumza katika uzinduzi huo ulifanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa kitengo cha huduma za M-Pesa kutoka Vodacom, Tulisindo Rashid akizungumza katika uzinduzi huo ulifanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Maendeleo ya Biashara na Masoko wa M-Pesa, Polycarp Ndekana, akizungumza katika uzinduzi wa halal pesa uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa kitengo cha huduma za M-Pesa kutoka Vodacom, Tulisindo Rashid (kushoto) wa pili ni
Meneja
mfawidhi huduma kwa wateja kutoka Amana Bank, Juma Msabaha wakiwa katika picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment