Na
Omary Mngindo, Bagamoyo
HALMASHAURI
ya wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, imevikopesha vikundi vya vijana, wanawake
na watu wenye ulemavu, kiasi cha shilingi milioni 57 kupitia mapato yake ya
ndani.
Katika
hafla fupi iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo chini ya
Mkuu wa wilaya Zaynabu Kawawa, taarifa ya Mkurugenzi Fatma Latu imeeleza
kwamba, halmashauri yao imetenga shilingi milioni 488.5 kwa ajili ya zoezi
hilo.
"Halmashauri
tunaendelea na utekelezaji wa sera kwa vitendo, ambapo kwenye maeneo ya
kiuchumi ikiwemo kilimo, ufugaji, biashara na sanaa, bajeti ya 2018/2019
tumetenga shilingi milioni 489,532, kati ya hizo milioni 248,911 ni asilimia
kumi ya mapato ya ndani," iloeleza taarifa ya Latu.
Imeongeza kwamba
katika mchakato huo kiasi cha shilingi milioni 240,421 ikiwa ni marejesho ya
mikopo ambayo vikundi mbalimbali vilikopeshwa kupitia ailimia 4 za wanawake, 4
za vijana huku mbili zikiwa za watu wenye ulemavu.
Kwa upande wake Kawawa alitanabaisha
kwamba kati ya fedha hizo za halmashauri shilingi milioni 57, imezinufaisha
vikundi vinne vya wanawake vilivyopewa milioni 16.3, vikundi vinane vya vijana
millioni 28.7 wakati kikundi kimoja cha watu wenye ulemavu kikipatiwa shilingi
milioni 2.5.
Aidha amewataka viongozi wa halmashauri zote mbili za Bagamoyo na
Chalinze kupitia maofisa maendeleo jamii kuwa naa utamaduni wa kuwapatia
mafunzo ya ujasiriamali wanavikundi, yatayowasaidia kitumia vema mikopo
wanayopatiwa ili Marengo ya serikali yafikiwe.
"Nitumie nafasi hii
kuwapongeza wote mlioona umuhimu wa kujiunga kwenye vikundi kisha kuomba mikopo
kutoka halmashauri, mtumie vizuri mikopo yenu ili mrejeshe kisha kuwapatia
fursa wengine kukopa, kumbukeni mikopo hii haina riba," alisema Kawawa.
Wakizungumza na waandishi wa habari baada ya zoezi hilo, Grace Vision Mhazini
vikundi cha Faraja alisema kuwa huo ni mikopo wa pili tangu waanzishe kikundi
hicho, huku wakiishukuru serikali kwa mikopo isiyokuwa na riba.
Nae mmoja wa
mwanakikundi cha wenye ulemavu Dunia Abdalaah alisema kwamba huo ni mkopo wao
wa kwanza wa shilingi milioni 2.5 tangu kuanzishwa kwake, ambapo wanajijusisha
na kilimo cha mpunga na ufugaji wa kuku.
No comments:
Post a Comment