Na
Shushu Joel.
WAZEE
wa Halmashauri ya chalinze wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani wamemtabilia Mbunge
wa jimbo hilo Ridhiwani Kikwete kuwa kuna siku anaweza akaja kuwa kiongozi
mkubwa wa nchi hii.
Utabili
huo wa wazee hao unatokana na jinsi Mbunge huyo anavyojituma katika utendaji
wake wa kuwaletea wananchi wa jimbo hilo maendeleo makubwa waliyokuwa
wakiyahitaji.
Wakizungumza
mara baada ya kikao cha kujadili maendeleo ya jimbo hilo wazee hao walisema
kuwa nguzo kubwa ya kiongozi bora ni unyenyekevu, upendo, mshikamano na utii
ambapo wamesema hizo zote Ridhiwani Kikwete anazo hivyo ni lazima atafika mbali.
Kwa
upande wake Shehe Lukatili ambaye ni kiongozi wa msikiti kata ya Miono alisema
kuwa Ridhiwani amekuwa msaada mkubwa kwao kutokana na vile utekelezaji wake wa
miradi ya maendeleo anavyoufanikisha kwa wananchi.
"Mie
kwa niaba ya wazee wenzangu wa kata ya Miono tunamuombea Mbunge wetu Ridhiwani
Kikwete aweze kuishi maisha marefu yenye baraka ili baadae aje kuwa kiongozi
mkubwa katika taifa hili "alisema.
Aliongeza
kuwa siku zote nyota njema uonekana asubui hivyo nyota ya kijana huyu imeanza
kuonekana na sie kama wazee tunamtakia kila la heri katika kuwatumikia
watanzania.
Naye
Muhammed Mzimba alisema kuwa Ridhiwani amekuwa kiongozi wa kuigwa na vijana
wengi hapa nchini kutokana na ujasiri wake wa kusimamia jambo na kulifanikisha
ili umma unufaike.
Aidha
aliongeza kuwa ufanikishaji wa miradi mikubwa kwenye jimbo lake la chalinze
kuna pelekea wazee na watu wengine jimboni kuona kuwa Ridhiwani ni mkombozi wa
Chalinze.
Kwa
upande wake Mbunge wa jimbo hilo Ridhiwani Kikwete alisema kuwa yeye hana
pingamizi lolote kwani wazee wanaona jinsi ninavyowapambania jimboni na pia ni
haki yao kumuombea kwa Mungu ili awafanikishie zaidi ya hapo.
Aliongeza
kuwa anaipongeza serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt John Pombe
Magufuli kwa juhudi zake inazozifanya kwa kuhakikisha chalinze inakuwa ni jimbo
lenye maendeleo ya kutosha.
"Kwa
kweli nakumbuka kipindi ambacho tulikuwa tukiomba kura mh Rais Dkt John Pombe
Magufuli alituambia wanachalinze watasahau shida na sasa yanaonekana kwani
serikali inaleta miradi mingi ya maendeleo chalinze ikiwemo umeme, huduma za
afya, miundombinu na sasa inapambana kumaliza changamoto za maji kwa jimbo
zima"Alisema Kikwete.
Aidha
amewataka wananchi kuendelea kuunga mkono juhudi za Dkt Magufuli kwani ni
kiongozi mwenye kupenda wanyonge.
No comments:
Post a Comment