Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Mhe.
Zainab Kawawa, akimpa dawa mtoto ikiwa ni uzinduzi wa chanjo uliofanyika Hospitali ya wilaya ya Bagamoyo.
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Mhe. Zainab Kawawa, akizungumza katika uzinduzi wa chanjo katika Hospitali wilaya Bagamoyo.
................................
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Mhe.
Zainab Kawawa, amefanya uzinduzi wa Wiki ya chanjo katika ukumbi wa
kliniki ya Mama na Mtoto wa Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo.
Uzinduzi huo uliofanyika jana May 3, 2019 ni wa
chanjo za Surua na rubella, nimonia kwa watoto wachanga, polio kwa watoto na
chanjo ya pepopunda kwa Wanawake wajawazito, zoezi lililosimamiwa na Mganga
Mkuu Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo, na wataalam wengine wa Afya ya mama na
mtoto katika Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo.
Akizungumza na Wanawake wajawazito na
wakina mama wenye watoto walio chini ya umri a miaka mitano waliohudhuria
kliniki hiyo ya mama na mtoto katika Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Kawawa amesema chanjo huokoa maisha ya mama na mtoto kwa kumkinga
dhidi ya maradhi ambayo yanazuilika, na kuongeza kuwa, kupata chajo ni jambo la
lazima kwa vile inalinda pia kizazi kijacho dhidi ya magonjwa mbalimbali kama
Surua na Polio.
“Ni wajibu na jukumu la kila Mzazi
kuhakikisha mtoto wake anapata chanjo mara baada ya kuelewa umuhimu wa chanjo,
Wakina Baba wasindikizeni kliniki wake zenu na wasisitizeni wakina mama
kuhakikisha wanapata chanjo zote kipindi cha ujauzito na wanapojifungua
hakikisheni mtoto aliyezaliwa anapatiwa chanjo zote za utotoni ili kumlinda na
maradhi kwani chanjo hizi ni salama na hazina madhara yoyote Kiafya”. Amesema
Mhe. Zainab.
Akifunga hafla hiyo ya uzinduzi wa
chanjo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Mhe. Alli Alli Issa
amemshukuru Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo kwa kufika na kutoa hamasa kwa Wanawake
ili waone umuhimu wa chanjo kwa watoto wao na kuahidi kwamba Halmashauri
itaendelea kuwahimiza Wakinababa kushiriki kwa kuwahimiza wakinamama kupata
chanjo zote wanapokuwa wajawazito na kusimamia mtoto atakayezaliwa ili apate
chanjo zake zote.
Huduma za chanjo zimeleta mapinduzi
makubwa katika kulinda afya ya jamii pengine kuliko huduma zozote za kitabibu
na hivyo kuokoa vifo vya mamilioni ya watu duniani kote.
Wiki ya chanjo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo inahusisha utoaji wa chanjo za Surua na rubela, pepopunda, polio, nimonia na chanjo ya saratani ya shingo ya kizazi kwa wasichana walio na umri kati ya miaka 9 hadi 14, na chanjo hizi zinatolewa katika Zahanati zote, Vituo vyote vya kutolea huduma za Afya na Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo.
Wazazi
waliofika Hospitali ya Bagamoyo kupeleka watoto wao kupata chanjo.
Mratibu
wa Chanjo wilaya ya Bagamoyo, Anna Chiganga akisoma taarifa mbele ya mgeni
rasmi wakati wa uzinduzi wa chanjo wilayani humo.
No comments:
Post a Comment