Na
Omary Mngindo, Lugoba
HALMASHAURI
ya Chalinze wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, imepokea wanafunzi wote 1,103
waliokosa nafasi ya kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza, kutokana na
upungufu wa vyumba 26 vya madarasa.
Idadi
hiyo kubwa ya wanafunzi hao imetokana na ufaulu mzuri wa wanafunzi hao uliochangiwa
na mkakati wa serikali kuhusu mpango wake wa elimu bure, unaolenga kuhakikisha
watoto wote wanapata haki ya msingi ya kupata elimu.
Hayo
yamebainishwa katika kikao cha Baraza la Madiwani robo ya kwanza kwa mwaka wa
2019, likiwa chini ya Mwenyekiti wake Said Zikatimu, Makamu Juma Mpwimbwi,
Mkurugenzi Mtendaji Amina Kiwanuka na wataalamu mbalimbali ambalo limeelezwa
kwamba vyumba 26 vimekamilika kwa sh. Mil. 522.
Zikatimu
alianza kwa kuwapongeza madiwani kwa kukubali kuidhinisha kiasi hicho cha fedha
kwa ajili ya zoezi hilo, huku akishukuru ushirikiano mkubwa kutoka kwa
wataalamu mbalimbali, sanjali na wananchi ambao wameungana katika kufanikisha
ujenzi huo.
"Nianze
kwa kuelezea furaha yetu ya kufanikisha ukamilishaji wa vyumba vyote 26 vya
madarasa, zoezi ambalo tumelifanikisha kupitia vyanzo vyetu vya mapato ya
ndani, wanafunzi wote 1,103 wameingia darasani wanaendelea na masomo yao,"
alisema Zikatimu. Wakichangia mada katika kikao hicho, diwani Hussein
Hading'oka amelalamikia ubovu wa barabara katani kwake, hiku aksema wakati
miundombinu hiyo ikisimamiwa naa halmashauri hali haikuwa hivyo.
"Katika
vijiji vyangu kuna ubovu mkubwa wa barabara, tangu kuingia kwa utaratibu mpya
wa barabara zetu kuwa chini ya TARURA kumekuwepo na matatizo makubwa, katika
kipindi hiki hazipitiki kabisa," alisema Hading'oka.
Aidha
halmashauri hiyo inenunua vifaa maalumu vya kupimia ardhi (GPS) vinavyolenga
lupungiza kama so kumaliza kabisa malalamiko ya upimaji wa ardhi ambapo katika
baraza lililopita diwani wa Kata ya Lugoba Rehema Mwene alilalamikia gharamaa
ya upimaji wa shamba eka moja kwa sh. Milioni moja.
Katika
baraza hilo Makamu Mwenyekiti Juma Mpwimbwi diwani wa Kata ya Miono, ameliomba
baraza hilo kuandaa mafunzo kwa vijana juu ya matumizi ya vifaa hivyo, ili
kuwarahisishia kazi hiyo wananchi na naofisa wanaohusika na idara hiyo.
No comments:
Post a Comment