Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma , Fatma
Toufiq, akieleza ushuhuda wake kwa waandishi wa habari juu ya ajali ilivyoweza
kumletea cahangamoto ya utendaji katika kazi.
Kaimu Mkurugenzi wa Chama cha Wanasheria
Wanawake Tanzania(TAWLA),Mary Richard akizungumza na Waandishi juu wiki ya
usalama barabarani
.....................................
Wito
umetolewa kwa Serikali na watunga sera kuhakikisha wanapitia upya na kufanya
mabadiliko katika sheria ya usalama barabarani ili kuweza kudhibiti ajali
zinazotokana na uzembe wa watu kwa makusudi.
Wito
huo umetolewa jijini Dar es Salaam leo Mei 05, 2019 na Kaimu Mkurugenzi wa Chama cha
Wanasheria Wanawake Tanzania(TAWLA),Mary Richard alipokuwa akizungumza na
Waandishi wa habari juu ya maadhimisho ya wiki ya usalama barabarani kwa umoja
wa mataifa.
“sheria
hiyo kwa sasa ina mapungufu mengi kiasi mtu akikutwa na kosa adhabu zake ni za
kawaida na makosa mengi yamebainishwa katika kanuni badala ya sheria yenyewe
ametaja sheria hii inamtaja mtu aliyekaa siti ya mbele na Dereva ndio wanapaswa
kufunga mkanda wakati kanuni inataja abiria wote wafunge mkanda jambo ambalo
lina ukakasi kidogo”amesema Mary.
Mary
ametaja kuwa sheria hii ya Sasa inaseama Dereva wa pikipiki ndio anapswa kuvaa
kofia ngumu peke yake wakati sasa jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani
wameweka kanuni Dereva na abairia ndio wanapaswa kuvaa kofia ngumu hivyo ni bora vitu
vyote hivi vingewekwa kwenye sheria ili utekelezaji wake ufanyike kwa mujibu wa sheria.
Aliongeza kwa kuomba mamlaka zinazohusika pamoja
na Wizara ya Mambo ya ndani waangalie utaratibu wa kubadilisha sheria hii ili kuendana na wakati na uhalisia wa matukio.
kwa
upande wake Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma , Fatma Toufiq amesema kuwa
ajali za barabarani zinaepukika kama watanzania wote wataweza kufuata sheria na
kuwa makini pindi wanapoendesha vyombo vya moto.
amesema
kuwa yeye kama mbunge anayeshiriki katika kutunga sheria atasimama kidete
kuhakikisha sheria hii mpya ya usalama barabarani inapatikana ili tuweze
kupunguza takwimu za ajali na walemavu wakudumu wanaotokana na ajali za
barabarani
No comments:
Post a Comment