Na
Shushu Joel, Busega.
WANAWAKE wa wilaya ya Busega mkoani Simiyu wamekili kuwa
Mbunge wa jimbo hilo Dr Rafael Chegeni ni kiongozi mwenye maono ya mbele
ikilinganishwa na watangulizi wake waliopita katika jimbo hilo.
Ujumbe huo
umetolewa jana na kina mama hao wakati walipokuwa wanakabidhiwa cherehani
ambazo walimuomba Mbunge huyo ili waondokane na tabia ya kuomba omba fedha
kutoka kwa waume zao huku nao wakiwa na fani zao.
Wakizungumza mara baada ya
kukabidhiwa cherehani hizo kina mama hao walisema kuwa Mbunge wao amewatoa katika
hatua ya kuwa tegemezi na kujiona kama wamezaliwa upya.
Akizungumza na
waandishi wa habari mmoja wa kina mama walionufaika na mradi huo Ng'washi Juma
alisema kuwa msaada huo umefika wakati mwafaka kutokana na uhitaji wetu kina
mama tuliokuwa tumeajiliwa na watu.
Aliongeza kuwa anatoa pongezi kwa Mbunge
huyo kutokana na jitihada zake za kuwakomboa kinamama ambao ndio chachu kubwa
ya maendeleo hapa nchini.
"Dr Chegeni amekuwa kiongozi shupavu na mwenye
kutambua mahitaji yetu kinamama kwani kipindi kirefu tulikuwa omba omba kutoka
kwa waume zetu lakini kutokana na misaada aliyokuwa akitupatia manufaa makubwa
"Alisema.
Naye mkuu wa wilaya hiyo Tano Mwera amempongeza Mbunge huyo kwa
kutambua thamani ya wanawake katika wilaya hiyo na hata kuwapatia vitendea kazi
ili waweze kujitegemea pasipo kutegemea waume zao.
Aidha alimtaka Dr chaegeni
kuongeza juhudi hizo ili kuwasaidia wanawake wa wilaya hiyo kwa kuwapatia
vitendea kazi zaidi na hata kufungua viwanda vya ushonaji. Kwa upande wake
Mbunge wa jimbo hilo Dr Rafael Chegeni alisema kuwa msaada huo ni moja ya
majukumu yake kwenye jimbo lake la Busega.
Hivyo amewataka kinamama hao
kuzitumia cherehani hizo kwa matumizi yaliyoyaomba ili kuwaletea mafanikio waliyokuwa
wakiyasubili kwa muda mrefu.
Aliongeza kuwa ameandaa mipango kabambe ya
kuhakikisha anawakomboa watu wa jimbo hilo na si tu kina mama bali kwa watu
wote ili kila mmoja awe na shughuli yake ya kumuingizia kipato.
Aliongeza kuwa
ametoa vifaa vyenye thamani ya zaidi ya milioni 7 kwa kinamama wasiopungua 30
kwa lengo la kuwatoa kwenye dimbwi la umasikini.
No comments:
Post a Comment