NA
HADIJA HASSAN, LINDI.
Zaidi
ya wanafunzi 50 wa kidato cha kwanza (C) wanaosoma katika shule ya sekondari
mingoyo Halmashauri ya Manispaa ya Lindi Mkoani Lindi wanalazimika kutumia maabara
ya Phizikia kama Darasa kufuatia changamoto ya madarasa iliyopo shuleni hapo.
Wakizungumza na BAGAMOYO KWANZA BLOG baadhi ya wanafunzi hao akiwemo Marijani Hamisi
mwajuma Adam na khalphan Jomary walisema kuwa changamoto wanayokutana nayo
wakiwa wanatumia madarasa hayo kuwa wanalazimika kuhama hama mara kadhaa katika
darasa lao pindi darasa hilo likitakiwa kutumiwa na wanafunzi wengine kwa ajili
ya kujifunza kwa vitendo.
“tunatumia darasa hili kutokana na changamoto ya
madarasa iliyopo shuleni kwetu lakini hata hivyo mara nyingine kama wanafunzi wa
darasa lingine wanataka kufanya practical sisi tunalazimika kuhama na kuhamia
darasa lingine hivyo inatuletea usumbufu na wakati mwingine tunapoteza muda wa
kujisomea kwa kutuhamisha hamisha” alisema Malijani Hamisi ambae ni miongoni mwa wanafunzi
hao
Nae khalphani jomary alisema changamoto nyingine wanayokumbana nayo wakiwa
wanatumia Darasa hilo kuwa hawako huru kulingana na mazingira yaliyokuwepo
katika darasa hilo akitolea mfano wa Viti na meza zinazotumika hazikupaswa
kutumika kwa muda mrefu.
“hivi viti tunavyotumia ni virefu zaidi , kwa namna
vilivyotengenezwa havikupaswa kutumika kwa zaidi ya vipindi viwili mfululizo
maana wakati mwingine vinatufanya tuhisi ganzi lakini hata hivyo kuendelea
kutumia darasa hili kwa siku nyingi bado sio salama kwa afya zetu kwa kuwa bado
kuna baadhi ya kemikali zinaendelea kuhifadhiwa katika chumba hiki" Alisema.
"Hebu fikiria
kama kukitokea mlipuko wa namna yoyote ile itakuwaje katika usalama wetu”
alihoji mwanafunzi huyo.
Kufuatia changamoto ya Madarasa
iliyopo katika Shule hiyo Serikali imetoa kiasi cha Tsh. Milioni 37.5 kwa ajili
ya kumalizia ujenzi wa vyumba vitatu vya Madarasa katika Shule hiyo Hali
iliyomfanya mkuu wa mkoa wa Lindi Godfrey Zambi kutembelea Shuleni hapo na
kuona Maendeleo ya ujenzi wa madarasa hayo na kuonyesha kurizishwa na ujenzi
huo.
Hata hivyo Zambi aliutaka uongozi wa Shule hiyo kuongeza kasi ya ujenzi wa
madarasa hayo ili yaweze kutumika kwa wakati.
Awali akitoa taarifa ya Shule hiyo
Mkuu wa Shule ya Sekondari Mingoyo Mwichande Lihoma alisema kuwa Shule hiyo kwa
sasa inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa vyumba 7 vya madarasa huku akisema kuwa
ujenzi wa Madarasa hayo matatu utasaidia kupunguza changamoto hiyo nasasa
kufanya upungufu wa vyumba vinne 4 vya madarasa.
Alisema kwa sasa ujenzi wa
vyumba hivyo vya madarasa umefikia asilimia 80 na tayari kati ya Tsh. Milioni
37.5 zilizotolewa na Serikali tayari SH. Milioni 26.4 zimeshatumika katika
ujenzi wa madarasa hayo
Muonekano
wa jengo la vyumba vya vitatu vya madarasa vinvyoendelea kujengwa katika shule
ya shule ya sekondari
mingoyo Halmashauri ya Manispaa ya Lindi Mkoani Lindi.
Picha na Hadija Hassan.
No comments:
Post a Comment