Na
Omary Mngindo, Kibiti
MBUNGE
wa Jimbo la Kibiti Mkoa wa Pwani Ally Ungando ameikabidhi shule ya sekondari ya
Zimbwini kompyuta 5 zenye thamani ya shilingi milioni 9.250,000.
Katibu wa
mbunge huyo Rajabu Mtwiku ameyasema hayo katika kikao cha Wazazi wa wanafunzi
wanaosoma kwenye shule hiyo, iliyoko Kata ya Kibiti kilichojadili maendeleo
ambapo wazazi na walezi walijitokeza kwa wingi kwa ajili ya uboreshaji wa elimu
shuleni hapo.
Kikao hicho kilichohudhuliwa na diwani wa Kata hiyo Hamidu
Ungando, mwishoni kulifanyika harambee iliyokusanya shilingi laki 418,000,
hatua inayounga mkono serikali ya awamu ya tano iliyoipatia shule hiyo shilingi
milioni 138 kwa ajili ya kuboresha vyumba vya madarasa.
Mtwiku aliwaambia
wazazi hao kwamba, mbunge wao Ungando ambaye alikabidhi kompyuta 5 za milioni
9,250,000, kaa sasa yupo katika majukumu ya bunge mjini Dodoma, na kwamba
amewaahidi kuendelea kuungana na wanajimbo hilo katika shughuli mbalimbali za
kimaendeleo.
"Mbunge anawasalimia, amesema yupo pamoja nasi katika
shughuli za kimaemdeleo, ikiwemo kugawa chakula na vitendea kazi wakati wa
mitihani ya kidato cha nne 2019 katika shule zote 12 kama anavyo fanya toka
aingie madarakani 2015," alisema Katibu huyo.
Kwa upande wake diwani
Ungando alisema kuwa harambee hiyo ya upatikanaji wa fedha hizo kiasi cha
shilingi 418,000 ni kuunga mkono jitihada za wazazi hao waliojenga vyumba
viwili kwa nguvu zao, hivyo kutimia vyumba 8 vipya vinavyo endelea kujengwa.
Katika mkutano huo diwani Hamidu ameunga mkono juhudi za wazazi hao kwa
kuchangia rimu 10, zenye thamani ya shilingi 120,000 kwa ajili ya matumizi ya
shule, huku akiahidi kuendelea kuchangia kila wakati ikiwa ni kuhakikisha
wanafunzi wanapata elimu stahiki.
Mmoja wa wazazi aliyejitambulisha kwa jina la
Said Mng'ombe amewataka wakazi wa Kibiti wabadilike na kutambua umuhimu wa
elimu, huku akisema kwamba wapo nyuma katika sekta hiyo, hivyo waungane
kuhakikisha shule infanya vizuri kitaaluma.
No comments:
Post a Comment