Mtakumbuka
kuwa 9 Aprili 2019 Serikali ilitoa Tamko la kusitisha matumizi ya Mifuko ya
plastiki hapa nchini ifikapo Juni Mosi 2019.
Katazo
hili linalenga kuepusha athari za kiafya na mazingira zinazoendelea kujitokeza
kutokana na matumizi ya mifuko hiyo.
Katazo hilo lililotolewa na Waziri Mkuu Mhe. Kasssim Majaliwa linahusu kupiga marufuku uzalishaji, uingizaji, usafirishaji nje ya nchi, usambazaji, uuzaji na matumizi ya mifuko ya plastiki ya aina zote.
Ofisi
ya Makamu wa Rais imekuwa ikitoa taarifa mbalimbali ili kuwaelimisha wananchi
kuhusu katazo hilo kupitia Vyombo vya Habari ikiwa ni pamoja na magazeti,
Runinga na Redio, Mitandao ya Kijamii, Mikutano ya wadau na kupitia mikusanyiko
ya watu ikiwa ni pamoja na taarifa kusomwa katika nyumba za ibaada.
Mpaka
sasa Serikali imetekeleza yafuatayo:
Ofisi ya Makamu wa Rais imeandaa Kanuni kuhusu Katazo hili.
Ofisi ya Makamu wa Rais imeandaa Kanuni kuhusu Katazo hili.
Kanuni
hizi zitaanza kutumika tarehe 1 Juni 2019. Kwa mujibu wa Kanuni hizi, itakuwa
ni marufuku kuzalisha, kuingiza nchini, kusambaza na kutumia mifuko ya plastiki
iliyotajwa katika Katazo hili.
Kiwanda,
Kikundi cha Watu au Mtu Binafsi atakayebainika kukiuka matakwa ya Kanuni hizi
atakuwa ametenda kosa la jinai na hivyo sheria itachukua mkondo wake.
Tumetoa
maelekezo Mahsusi kwa Sekretariet za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa
kuhusu utekelezaji wa katazo hii ambapo baadhi yao wameanza kutenga maeneo
maalumu kwa ajili ya uhifadhi wa shehena ya mifuko itakayosalimishwa.
Kwa
kushirikiana na Makampuni ya Simu ya Vodacom, Tigo, Airtel na Halotel
tumefanikiwa kutuma ujumbe mfupi kwa njia ya simu kwa watumiaji wa mitandao
hiyo ambapo watumiaji milioni 11 wa Tigo, Milioni 15.5 wa Vodacom wameshapata
ujumbe huu, hii itakuwa endelevu kila wiki.
Tumeandaa
na kusambaza taarifa kwenye taasisi za dini ili nao watusaidie kufikisha ujumbe
huu kwa waumini wao, tunawashukuru sana wameitikia wito vizuri.
Tumekutana
na wazalishaji wa mifuko mbadala wa plastiki na wamepanga kuongeza kasi zaidi
uzalishaji wa bidhaa hii na baadhi wameshaagiza mitambo ya kuzalisha mifuko
mbadala.
Tunaendelea
kutoa matangazo kwa kutumia vipaza sauti katika ngazi ya Kata, Mitaa na Vijiji
kila wiki
Tumeendelea kutoa elimu kupitia Vyombo vya Habari ikiwa ni pamoja na kufanya Media Tour, kutoa ‘Count down’ kwenye magazeti, kutumia redio za kijamii na redio za mikoani kutoa matangazo juu ya katazo hili.
Tumeendelea kutoa elimu kupitia Vyombo vya Habari ikiwa ni pamoja na kufanya Media Tour, kutoa ‘Count down’ kwenye magazeti, kutumia redio za kijamii na redio za mikoani kutoa matangazo juu ya katazo hili.
Pia
tumetumia mitandao ya kijamii (Tovuti, blogs, facebook, twitter na istagram)
bila kusahau katuni ili kuhakikisha ujumbe unafika kote.
Tumetengeneza
Bronchure, fliers, Banners na stickers na tunahakikisha tunawasambazia watu
wote ili wapate uelewa ikiwa ni pamoja na wasafiri katika Vyombo vya usafiri
Tunaendelea
na utoaji wa Makala maalumu katika magazeti na kutumia redio kurusha matangazo
yetu.
Jitihada
zote hizi zinapaswa kuungwa mkono na si kubezwa, pia nitoe rai kwa watanzania
wote kutopotosha jambo hili kama ilivyofanywa juzi katika kipande cha video
(Clip) iliyosambazwa katika mitandao ya kijamii.
Na
kipande hiko ni cha mwaka jana 2018 wakati wa kikao kilichoandaliwa na Ofisi ya
Makamu wa Rais kuzungumza na Wadau wa mifuko.
Ikumbukwe
kuwa ifikapo tarehe 1 Juni 2019, Serikali itaendesha operesheni kabambe nchi
nzima ya kusaka mifuko hii.
Operesheni
hii itahusisha Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Kamati za Ulinzi na Usalama za
Mikoa na Wilaya, Mamlaka za Serikali za Mitaa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu
wa Serikali, Shirika la Viwango la Taifa (TBS), Mamlaka ya Chakula na Dawa
(TFDA), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, pamoja na Mamlaka za Viwanja vya Ndege,
Bandari, Forodha, Uhamiaji, na Usafiri wa Nchi Kavu.
Kwa
wale ambao watakuwa tayari kusalimisha kwa hiari shehena ya mifuko watakayokuwa
nayo, utaratibu utatolewa wa mahali rasmi wanapotakiwa kuisalimisha kwenye
maeneo yao.
Kwa
taarifa zaidi kuhusu utekelezaji wa katazo hili Wananchi kwa ujumla mnashauriwa
kutembelea Ofisi za Kanda za Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa
Mazingira (NEMC) zilizopo Dar es Salaam, Mtwara, Dodoma, Mbeya, Mwanza, Kigoma
na Arusha.
Aidha,
wanaweza pia kuwasiliana na Wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa Miji
na Wilaya.
Nirudie
tena kutoa rai kwa Watanzania wote kuzingatia maelekezo haya ya Serikali pamoja
na matakwa ya Kanuni za kupiga marufuku matumizi na biashara ya mifuko ya plastiki
nchini kwa mustakabali wa uhifadhi wa mazingira ya nchi yetu.
Asanteni
kwa kunisikiliza,
Imetolewa na:
Imetolewa na:
Balozi Joseph E. Sokoine
NAIBU KATIBU MKUU, OFISI YA MAKAMU WA RAIS
11 MEI, 2019
NAIBU KATIBU MKUU, OFISI YA MAKAMU WA RAIS
11 MEI, 2019
No comments:
Post a Comment