MBUNGE
wa jimbo la chalinze wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Ridhiwani Kikwete, akifungua kitambaa kama ishara ya uzinduzi wa Hosteli ya wasichana katika shule ya sekondari Mboga iliyopo katika Jimbo lake.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Mboga Halmashauri ya Chalinze wakisalimiana na Mbunge wa jimbo hilo, Ridhiwani Kikwete wakati wa uzinduzi wa Hosteli ya wasichana katika shule hiyo.
...............................................
Na
Shushu Joel, chalinze.
MBUNGE
wa jimbo la chalinze wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Ridhiwani Kikwete
amewataka wanafunzi wa sekondari katika jimbo lake kusoma kwa bidii masomo ya
sayansi kutokana na uharaka wa upatikanaji wa ajira kwenye fani hiyo.
Rai
hiyo ameitoa alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Mboga
mara baada ya uzinduzi wa majengo ya hostel kwa wasichana shuleni hapo .
"Masomo
ya sayansi yana nafasi kubwa katika ajira na hasa katika serikali ya viwanda
kutokana na uzalishaji mwingi ni wa kisayansi hivyo tuchangamkie nafasi ya
kusoma masomo hayo " Alisema Kikwete.
Aliongeza
kuwa kutokana na kukua kwa technologia duniani wanasayansi wamekuwa
wakihitajika kila siku hivyo juhudi za ufundishaji wa masomo hayo iongezeke ili
kuwafungulia fursa watoto wetu wa chalinze.
Mbali
na hilo Kikwete amewataka wanafunzi kuzingatia masomo kwani wazazi na walezi
wamekuwa wakijibana katika matumizi yao ya kila siku ili kuhakikisha wanasomo
na kuja kuwakomboa baadae hivyo muda wautumie ipasavyo ili kufanikisha malengo
yao ya baadae.
"Ni
aibu msichana kukatisha masomo yako kwa ujauzito na pia aibu kwetu wazazi hivyo
nawataka msidanganyike na wavulana katika kipindi hiki cha masomo yenu, pia
hata wavulana kuwekwa ndani na kinamama wenye uwezo ingawa kesi hii ni ndogo
kuliko ya wasichana kukatishwa masomo yao na wanaume".
Aidha
amewataka wavulana kuwa na subra kwani bado anakusanya nguvu za kumalizia
majengo yao matatu ya hostel ili nao waweze kuhamia shuleni hapo kwa kusudi la
kuendelea kupiga kitabu.
Omary
Adam ni mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule hiyo amempongeza Mbunge huyo
kwa juhudi zake za kupambana na elimu katika jimbo hilo ili uzalishaji wa
wasomi jimboni humo uweze kuwa mkubwa.
Aliongeza
kuwa kwa upande wa wasichana wao tayari majengo yao yamekamilika na wamesha
anza kutumia lakini yetu wavulana bado kupauliwa hivyo kama ukipata wafadhili
na sie utukumbuke ili kupunguza nafasi za kwenda na kurudi nyumbani nasi tuwe
tunabaki kama wasichana.
Naye
Amina Ally amemshukuru Mbunge huyo kwa kutambua thamani ya watoto wa kike na
kuona changamoto zao zilizokuwa zikiwakabili na kuzitatua kwa haraka.
Hivyo
kutokana na wasichana Kulala shuleni ufaulu utaongezeka kwa asilimia kubwa
kwani vishawishi tulivyokuwa tukivipata njiani havitakuwepo tena.
No comments:
Post a Comment