NA
HADIJA HASSAN, LINDI.
Mkuu
wa mkoa wa Lindi Godfrey zambi ameliagiza jeshi la Polisi Wilaya ya Lindi
kumkamata Mkazi wa kata ya Chikonji Halmashauri ya Manispaa ya Lindi Mkoani
humo ISMAIL HASSAN kwa kosa la kukutwa anacheza pooll table nyakati za
Asubuhi pamoja na kuwasaka wamiliki wa pool Table hiyo Abdallah Ally Jadu.
hayo
yametokea mai 9 mwaka huu majira ya saa nne Asubuhi ambapo mkuu huyo wa Mkoa
alikuwa katika ziara yake ya kutembelea Miradi ya TASSAF katika mtaa wa
Nanyanje na Jangwani Halmashauri ya manispaa ya Lindi.
Akiwa anaelekea katika
mradi huo ndipo alikuta baadhi ya Vijana wa kata hiyo wakicheza mchezo huo wa
Pooll Table nyakati za Asubuhi hali ya kuwa Serikali ilishapiga marufuku
michezo hiyo kuchezwa nyakati za Asuhuhi hasa katika siku za kazi.
Zambi
alionyesha kuchukizwa na kitendo hicho huku akisema kuwa kijana huyo ataendelea
kushikiliwa na Jeshi la polisi kuwataja wenzake aliokuwa akicheza nao mchezo
huo pia liwe fundisho kwa vijana wengine wenye tabia kama yake.
Aidha, Zambi pia
pamoja na mambo mengine aliamuru jeshi hilo la polisi kuharibu meza hiyo ya
pooll kwakuzivunja vunja.
“tumekuwa tukisema mara kwa mara sio ruhusa kucheza
pooll table nyakati za asubuhi lakini kunawatu wanajaribu kukaidi maagizo
yanayotolewa na Serikali sasa nyinyi mnachukuliwa ili iwe fundisho kwa wengine
maana hatuwezi kuendelea kuishi kwa namna hii , haiwezekani tuseme kila siku
yale yale sasa kwa sababu huku kuna watu wananchi yao basi wanaishi wanavyotaka
wao kucheza pooll asubuhi maana yake mnaendekeza uvivu” alisisitiza zambi.
Akihojiwa na BAGAMOYO KWANZA. Ismail Hassan ambae ameshikiliwa na jeshi la
polisi alisema kuwa amesikitishwa na kitendo cha Mkuu huyo wa Mkoa kuagiza
ashikiliwe na jeshi hilo badala ya viongozi wa serikali ya mtaa ambao ndio
walikuwa na wajibu wa kusimamia michezo hiyo isifanyike.
“Mimi nimeshikwa tuu
ndugu muandishi lakini kwanza mimi ni mgeni katika maeneo hayo nimekuja tuu kwa
muda lakini toka nimefika hapo miezi miwili iliyopita nimekuwa nikishuhudia
mchezo huu ukiendelea nikajua huu ndio utaratibu wao waliojiwekea, kama
viongozi wa mtaa wangefanya majukumu yao kwa ufasaha hata mkuu wa mkoa
asingeweza kukuta mchezo huu unachezwakwa wakati huu hivyo mimi sina kosa
katika hili” alisema Hassan.
No comments:
Post a Comment