Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Taasisi
ya The Islamic Foundation Aref Nahdi, katika ni Naibu balozi wa umoja wa falme za kiarabu UAE
Mohamed Ibrahim Al bahri, na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Mkaonda, wakati wa zoezi la kugawa vyakula lililofanyika jijini Dar es Salaam.
.....................................
Taasisi ya The Islamic Foundation
(TIF) yenye makao yake makuu Mkoani Morogoro nchini Tanzania, kwa kushirikiana na
Umoja wa nchi za falme za kiarabu UAE wametoa msaada wa vyakula wa tani Zaidi
ya 40 kwa watu Zaidi ya 700 wasiojiweza.
Walengwa wa msaada huo ni wazee,
wajane, watu wenye ulemavu pamoja na watu wenye uhitaji, katika kipindi hiki
cha Mwezi wa Ramadhani.
Msaada huo umetolewa jijini Dar es
salaam na kushuhudiwa na Mkuu wa Mkoa huo, Paul Mkaonda pamoja na Sheikh wa Mkoa huo Alhad Mussa Salum.
Vyakula vilivyotolewa kwa kila
mlengwa ni pamoja na mchele kg20 unga wa sembe kg20
maharage kg10 sukari kg5 pamoja na mafuta ya kupikia lita 3.
Naibu balozi
wa umoja wa falme za kiarabu UAE Mohamed Ibrahim Al bahri ameikabidhi Taasisi ya
The Islamic Foundation (TIF) huku akishuhudia ugawaji ukifanyika kwa
walengwa.
Akizungumza na wanahabari katika
zoezi hilo la ugawaji wa msaada naibu balozi wa umoja wa falme za kiarabu UAE
Mohamed Ibrahim Al bahri, amesema kuwa msaada huo ni moja kati ya miradi wanayo
itekeleza kwa nchi ya Tanzania lengo likiwe ni kuweza kutoa ushirikiano wa
karibu kwa serikali katika kuwahudumia wananchi wa Tanzania katika masuala ya
huduma za kijamii ikiwemo kutekeleza miradi ya kutibu moyo watoto wadogo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi
ya The Islamic Foundation Aref Nahdi amesema kuwa msaada huo ni juhudi za Taasisi
ya The Islamic Foundation (TIF) za utekelezaji wa miradi wanayopatiwa na
wahisani na wao kuwafikishia wahitaji kwa wakati.
Alisema Taasisi hiyo imekuwa ikitekeleza
shughli mbalimbali za kufikisha mahitaji kwa watu wanaokusudiwa hali
inayopelekea kujenga uaminifu kwa wahisani dhidi ya Taasisi hiyo.
Alifafanua kuwa, katika kugawa
misaada mbalimbali chini ya Taasisi ya The Islamic Foundation (TIF) yapo mambo
yanayozingatiwa ili malengo ya watoaji yafikiwe kwa kuwakabidhi walengwa.
Alibainisha kuwa, katika uislamu kuna
zaka na sadaka ambapo sadaka hupewa mtu yeyote mwenye uhitaji huku zaka
ikitakiwa kutolewa kwa makundi maalum ambayo yame ainishwa katika Qur ani.
Akielezea historia ya The Islamic
Foundation katika kutoa misaada ya aina hiyo, Aref alisema hiyo si mara ya
kwanza kugawa misaada na kwamba hiyo inatokana na kuaminika na wahisani wa ndani
na nje ya nchi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul
Makonda akizungumza katika zoezi hilo liloandaliwa na Taasisi ya The Islamic
Foundation (TIF) amewataka viongozi wa dini kuzidi kusimamia Amani ya nchi.
Aidha amepongeza ushirikiano huo wa
Falme za Kiarabu pamoja na nchi ya Tanzania ambao unasaidia kuimarisha
mahusiano.
Vyakula hivyo kama vinavyoonekana pichani, ambapo mtu mmoja ameweza kufungashiwa mchele kg20 unga wa sembe kg20
maharage kg10 sukari kg5 pamoja na mafuta ya kupikia lita 3.
Magari yaliyobeba vyakula hivyo yakiwa Makao Makuu ya Taasisi ya The Islamic Foundation (TIF) mjini Morogoro kabla ya kuanza safari ya kwenda jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment