Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais
(Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba (katikati) akizungumza na
wazalishaji wa mifuko mbadala wa plastiki (hawapo pichani). Katika kikao
kilichofanyika katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam, pamoja na mambo
mengine wazalishaji hao wa mifuko mbadala wameihakikishia Serikali kuwa wako
tayari kuongeza kasi ya usambazaji wa mifuko mbadala kote nchini, Kushoto ni
Mkurugenzi Mkuu Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira Nchini
Dkt. Samuel Gwamaka. Kulia Dkt. Freddy Manyika Kaimu Mkurugenz Idara ya
Mazingira.
Sehemu ya wazalishaji wa mifuko mbdala wa
plastiki kutoka Kampuni mbalimbali wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu
wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba (hayupo pichani) katika
kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam, pamoja na
mambo mengine wazalishaji hao wa mifuko mbadala wameihakikishia Serikali kuwa
wako tayari kuongeza kasi ya usambazaji wa mifuko mbadala kote nchini ikiwa ni
utekelezaji wa agizo la Serikali la kusitisha matumizi ya mifuko ya plastiki
hapa nchini ifikapo tarehe 1 Juni 2019.
Bw. Heneriko Batamuzi kutoka Kampuni ya Kenwood
Enterprise (T) Ltd akichangia mada katika kikao cha wadau cha kupitia Rasimu ya
Kanuni za kusimamia Taka Hatarishi hapa nchini. Ofisi ya Makamu wa Rais
imeandaa rasimu ya Kanuni mpya za kusimamia Taka Hatarishi nchini ikiwa ni
pamoja na ukusanyaji, urejelezaji, uteketezaji na usafirishaji wake ndani na
nje ya nchi. Kikao hiki kimefanyika katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es
Salaam.
No comments:
Post a Comment